KLABU ya Chelsea itamsaini Samuel Eto’o
kwa Mshahara wa Pauni Milioni 7 kwa mwaka leo Alhamisi baada ya kukubali
matokeo ya kumkosa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Eto’o, mshambuliaji wa Cameroon mwenye
umri wa miaka 32 amekubali malipo hayo kidogo kutoka Pauni Milioni 17
alizokuwa akilipwa Anzhi Makhachkala kwa mwaka na kumfanya awe mchezaji
anayelipwa zaidi duniani na atasaini kama mchezaji huru.
Pamoja na hayo, inafahamika Anzhi imemlipa mamilioni Eto’o ya Pauni ili kuvunja naye Mkataba.
Kifaa kinawasili: Samuel Eto'o akiwasili Stesheni ya Treni ya St Pancras jana usiku tayari kukamilisha uhamisho wake Chelsea
Ndani ya Treni: Eto'o, anayetarajiwa kupata mshahara wa chini Chelsea, akiwa ndani ya Treni baada ya kutua St Pancras jana usiku
Suluhisho? Samuel Eto'o anatua Chelsea kumaliza tatizo la safu ya ushambuliaji kwa Jose Mourinho
Mlengwa: Mourinho amemkosa Wayne Rooney wa Man United
REKODI ZA MAGWIJI CHELSEA KABLA YA SAMUEL ETO'O
Chelsea imewahi kusaini wachezaji wakongwe kabla ya Eto'o na imepata matokeo tofauti. . .
George Weah
Mchezaji
bora zaidi daima Afrika alitua mwaka 2000 kutoka AC Milan, akiwa na
umri wa miaka 33. Hakupewa nafasi sana chini ya kocha Gianluca Vialli,
licha ya kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza na Spurs.
MATOKEO: Alifeli.
Gianfranco Zola
Alitua
London mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 30 na katika mechi 312
alifunga mabao 80, na kujitengenezea heshima kubwa darajani.
MATOKEO: Alifanikiwa.
Gianluca Vialli
Akiwa
na umri wa miaka 32-alikataa kujiunga na Rangers na kusaini kikosi cha
Ruud Gullit mwaka 1996. Lilikuwa dau kubwa la Pauni 600,000 na Vialli
akaenda kufunga mabao 40 katika mechi 78, kisha akaeukia kuwa kocha
mwenye mafanikio.
MATOKEO: Alifanikiwa.
Pop Robson
Gwiji
huyo wa Newcastle na West Ham alijiunga na Chelsea akiwa na umri wa
miaka 36 mwaka 1982. Alifunga katika mechi yake ya kwanza, lakini
akafunga mabao mawili tu zaidi akiwa kocha na mchezaji.
MATOKEO: Alifeli.
Andriy Shevchenko
Milan
ilisikitika wakati Sheva anaondoka akitimiza miaka 30 kwa dau la Pauni
Milioni 30.8. Lakini mashabiki wa Chelsea muda si mrefu walijutia
usajili wa mshambuliaji huyo wa Ukraine, ambaye aliishia kufunga mabao
22 katika misimu mitatu.
MATOKEO: Alifeli.
Eto'o aliwasili katika Stesheni ya Treni
ya London, St Pancras usiku wa jana na anatarajiwa kufanyiwa vipimo
katika viwanja vya mazoezi vya Chelsea, Cobham kabla ya kukamilisha
usajili wake leo.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho,
alithibitisha kumfanya Eto’o mchezaji wa pili anayemzikia na mpango wake
B baada ya United kugoma kumuuza Rooney.
Kwa sasa, mshambuliaji huyo wa England
ameamua kuendelea na maisha Old Trafford baada ya kuandika katika
ukurasa wake wa Facebook kuwashukuru mashabiki kwa mapokezi mazuri
wakati United ikimenyana na Chelsea na kutoa sare ya bila kufungana
usiku wa Jumatatu.
Rooney aliposti: "Ilikuwa vigumu kuamini
namna mashabiki walivyofanya, nawashukuru mno. Hakika nakubali sapoti
yenu. Inamaanisha mengi,".
Mourinho anaweza kujaribu tena baadaye
msimu huu kuinasa saini ya Rooney, lakini kwa sasa anamaliza shida zake
kwa Eto’o, ambaye aliwahi kumzungumzia kwamba: "Kocha yeyote atakuwa
mpumbavu kutotaka kuwa na mshambuliaji kama yeye,".
Kuna mambo makubwa yanatarajiwa kutokana na kocha huyo wa Chelsea na mchezaji wake huyo mpya.
Eto’o hajawahi kwenda tofauti na
matarajio. Akiwa Barcelona, alikamata kipaza sauti katika matangazo ya
moja kwa moja ya Televisheni na kuikandia klabu yake ya zamani, Real
Madrid ‘b*****ds’ kushangilia taji la Barcelona la ubingwa wa Hispania
mwaka 2005; aliwahi pia kuponda hadharani kiwango cha chini cha
Ronaldinho na aliwahi kuondoka uwanjani baada ya mashabiki jukwaani
kuanza kumfanyia hila za kibaguzi katika mechi na Zaragoza.
Ajabu pamoja na urafiki wake na Mourinho kwa sasa, lakini wametokea kuwa adui kiaina fulani.
Alipokwenda Stamford Bridge mwaka 2005
wakati Chelsea ilipoifunga Barcelona katika Ligi ya Mabingwa, Eto’o
alitoa maoni yake akikandia mbinu za kiuchezaji za Chelsea. Mourinho
anapenda uimara wa mchezaji huyo.
"Nilipenda ukweli kwamba anafanya kazi kwa kujituma,"alisema Mourinho.
Wawili hao baadaye waliuangana Inter
Milan ambako Eto’o alimuwezesha Mourinho kushinda mataji matatu ndani ya
msimu. Wakati huo, Mwanasoka huyo bora mara nne Afrika alifunga bao
pekee la ushindi Stamford Bridge na kumaliza matumaini ya Chelsea katika
Ligi ya Mabingwa.
Wanaungana tena: Eto'o na Mourinho walitwaa mataji matatu Inter Milan mwaka 2010
Maswali tu ni kwamba bado ana kasi ile
ile iliyomfanya tishio kwa wapinzani Italia na Hispania na kulikuwa kuna
ushahidi mwaka jana katika Ligi ya Urusi na Ulaya, Europa League kwamba
kasi yake inapungua sambamba na kuongezeka kwa umri wake.
Pamoja na hayo, shaka juu ya kasi yake
inaondolewa na uhusiano wake na mchezaji mpya mwingine wa Chelsea kutoka
Anzhi, Mbrazil Willian, ambao umekuwa ukizalisha mabao japo moja katika
mechi mbuili. Ni bahati nasibu Mourinho anacheza kumsajili Eto’o.
"Kuna Jose Mourinho mmoja tu," Eto’o
aliwahi kusema wakati fulani juu ya kocha wake huyo wa zamani.
"Nimecheza chini ya makocha wengi wakubwa, lakini hakuna mtu mfano wa
Jose katika katika mchezo huu,".
Pio: Mourinho amemkosa mshambuliaji wa United, Rooney
Alichoandika kwenye ukurasa wake: Wayne
Rooney ametumia ukurasa wake wa Facebook kuwashukuru mashabiki wa Old
Trafford kwa sapoti waliyompa kwenye mechi dhidi ya Chelsea
"Ningependa kupata nafasi ya kucheza chini yake tena, kwa sababu haijawahi kuboa napokuwa karibu na Jose,".
Kutua kwa Eto’o ni kama pigo kwa
washambuliaji wa tatu wa timu hiyo ya Stamford Bridge. Fernando Torres
na Romelu Lukaku walikuwa benchi Old Trafford usiku wa Jumatatu na Demba
Ba, anayetakiwa kurejea Newcastle na kocha Alan Pardew, hakuwamo kabisa
kikosini.
Kutua kwa Willian na Eto’o haiwezi kuwa
dalili za Chelsea kumaliza kununua wachezaji, kwani klabu hiyo pia ipo
kwenye mazungumzo na Porto juu ya Christian Atsu, winga mwenye thamani
ya Pauni Milioni 4, ambaye pia aliwahi kutakiwa na Cardiff, Tottenham na
Liverpool. Na mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ghana chini ya umri wa
miaka 21 kuna matumaini makubwa akaungana na magwiji wa Chelsea.
Lakini iwapo watafanikiwa kumsaini Atsu
mbele ya Spurs walioamua kumwaga fedha sokoni, litakuwa pigo la pili kwa
Andre Villas-Boas majira haya ya joto, kufuatia kuzidiwa kete kwa
Willian.
Wote tabasamu: Kiungo wa Brazil, Willian amefurahia kukamilisha usajili wake Stamford Bridge
0 comments: