Hata hivyo, Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe alionyesha kutoafiki kuombwa kwa Rais Museveni
akisema naye yuko katika kundi linaloitenga Tanzania.
Kauli ya kwamba Tanzania kupitia kwa Rais Kikwete
imemuomba Rais Museveni kuwa msuluhishi wa mgogoro huo,ilitolewa jana
bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali
la papo kwa hapo aliloulizwa na Mbowe akitaka kupata kauli
ya Serikali juu ya kuibuka kwa mgogoro huo wa kidiplomasia na dalili za Tanzania kutengwa.
ya Serikali juu ya kuibuka kwa mgogoro huo wa kidiplomasia na dalili za Tanzania kutengwa.
Katika swali lake la msingi, Mbowe alisema mvutano
huo wa kidiplomasia umesababisha Tanzania kutengwa katika shughuli
ambazo zilipaswa kuwa za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alikiri kuwapo kwa
hali ya kutoelewana na kwamba hata baada ya kauli ya Rais Kikwete kuwa
Tanzania haina uhasama na Rwanda, mvutano unaendelea.
“Mimi ninavyojua Rais (Kikwete) amemuomba Rais wa
Uganda Yoweri Museveni ajaribu kuona ni namna gani jambo hili linaweza
kusuluhishwa na maneno haya yakapungua,” alisema Pinda.
Waziri Mkuu alisema anaamini busara zitatumika ili
kuona jambo hilo linakwisha vizuri lakini kama litaendelea na kuonekana
dalili za Tanzania kutengwa busara zaidi itahitajika. Katika swali la
nyongeza, Mbowe alisema kinachoonekana, Rwanda wameweza kuwavuta Waganda
na Wakenya katika mikakati ya kiuchumi ambao kwa hali ya kawaida
ingekuwa ni ya jumuiya
Alisema viongozi wa mataifa hayo wamekutana Kampala na Kenya bila kuwapo kwa Tanzania.
0 comments: