TUHUMA ZA SYRIA KUTUMIA SILAHA ZA KEMIKALI NI UPUUZI MTUPU'' RAIS VLADIMIR PUTIN WA URUSI


Putin
Rais Vladimir Putin wa Urusi anasema tuhuma kuwa serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali ni upuuzi mtupu.
Anasema jeshi la Syria lilikuwa linasonga mbele, hapakuwa na sababu ya serikali kuwapa kisingizio wale wanaotaka kuingia kijeshi.
Bwana Putin alisema ikiwa Marekani ina ushahidi kuthibitisha tuhuma zake, basi ikabidhi ushahidi huo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa.
Alimkumbusha Rais Obama kuwa aliwahi kutunzwa tuzo ya amani ya Nobel, na alimsihi kuwakumbuka wanyonge katika mashambulio.
Alikaribisha uamuzi wa bunge la Uingereza ambalo halikuunga mkono Uingereza kuingilia kati Syria, na anasema ameshangazwa na uamuzi huo wa bunge.
Share on Google Plus

0 comments: