MAN UTD, L'POOL LEO HAPATOSHI ANFIELD


London, England. Kocha David Moyes ataiongoza Manchester United kuifuata Liverpool kwa mara ya kwanza leo kwenye Uwanja wa Anfield, huku Arsenal wakiwakaribisha Tottenham Spurs.
Moyes aliondoka Everton na kuchukua mikoba ya Sir Alex Ferguson msimu huu, lakini sasa anarejea Merseyside ikiwa ni baada ya michezo mitatu msimu huu.
Kikosi chake cha United kimekuwa na matokeo ya kuvutia wakishinda moja, sare dhidi ya Chelsea Jumatatu.
“Anfield ni sehemu ngumu wakati wote,” alisema Moyes. “Ni uwanja mzuri nimejiandaa kurudi hapo, najua hali inavyokuwa unapocheza kwenye uwanja ule ni wazi mechi itakuwa ngumu na ushindani kama inavyokuwa wakati wote, ni matumaini yangu tutaondoka
na pointi tatu muhimu. Liverpool ni moja ya timu bora katika msimu huu.
“Kila mtu ananiambia kuhusu ushindani uliopo kati ya Liverpool na United, ni kama ilivyokuwa kwa Everton. Nimejiandaa kwa mchezo na nimekuja na Manchester United vyote vivyohusu mechi ya aina hii najua.”
Liverpool inaingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri ya ushindi pamoja na kumkosa mshambuliaji wao aliyefungiwa Luis Suarez.
Daniel Sturridge amechukua jukumu la ufungaji kwa kufunga michezo yote miwili waliyocheza awali. Wakiwa na pointi sita katika michezo miwili kunawafanya vijana wa Anfield kujiamini zaidi, nahodha Steven Gerrard ni matumaini yake kasi yao ya ushindi wataiendeleza leo.
“Kwa kipindi kirefu tofauti kati yetu na United, Chelsea na sasa Manchester City imekuwa ni kubwa,” alikiri Gerrard. “Kila mwaka tunajaribu kupunguza pengo hilo, nadhani msimu huu tutarudisha heshima yetu
Share on Google Plus

0 comments: