MANDELA HAKUTOLEWA HOSPITALI BADO MAHTUTI JAPO HALI YAKE IMETULIA KIDOGO

Serikali ya afrika Kusini imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba aliyekuwa kiongozi wa afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye amelazwa hospitali tangu mwezi wa Juni, kwamba alirejeshwa nyumbani Johannesburg Ijumaa usiku.
Taarifa ya serikali imesema
kuwa Bwana Mandela bado yuko hospitali mjini Pretoria na kwamba bado mahtuti, lakini hali yake imetulia.
Kulazwa kwa muda mrefu kwa kiongozi huyo kumewatia wasiwasi raia wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla.
Mandela ambaye ana umri wa miaka 95, alikuwa Muafrika wa kwanza kuwa rais wa taifa la Afrika Kusini, na anaheshimiwa na wengi kama baba wa taifa.
Share on Google Plus

0 comments: