BONDIA WA MAREKANI ATAMBA KUMSAMBARATISHA BONDIA CHEKA KESHO DIAMONDI JUBILEE

Bondia Phil Williams wa marekani akiwa na mkanda wake wa ubingwa wa WBU mara baada ya kuwasiri nchini
WAKATI bondia wa nchini Marekani, Phil Williams akipima uzito leo, amejigamba kumfanyia kitu mbaya mpinzani wake Francis Cheka. Pambano hilo la kuwania ubingwa wa Dunia, limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Rais wa TPBO, Yassin Abdallah alisema mpinzani wa Cheka
amewasili na wapambe wake, huku akijitapa kumfundisha adabu Cheka.

Bondia Phil Williams wa marekani

“Mmarekani amepania kumtwanga Cheka na kumfundisha jinsi ya kupigana, hivyo ni pambano la kihistoria,” alisema.

Alisema kuwa mgeni rasmi kwenye pambano hilo ni bingwa wa Dunia wa Uzito wa juu wa zamani, Francois Botha ‘White Buffalo.
Mdau wa michezo nchini Saidi kindeka kushoto akiwa na Bondia Phil Williams wa marekani
Share on Google Plus

0 comments: