CHADEMA WANATAKA KUVUNJA UNDUGU NA MSHIKAMANO WA WATANZANIA'' NGOMBALE MWIRU


Ngombale Mwiru, amepingana wazi wazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuhusu rasimu ya Katiba mpya. Mwanasiasa huyo, ambaye ametumikia Serikali kwa nyadhifa mbalimbali na katika vipindi tofauti pamoja na chama hicho kikuu cha
upinzani nchini, wameonesha kutofautiana kimsimamo katika kipengele cha muundo wa Serikali.


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
Wakati Chadema ikipigia debe muundo wa serikali tatu, kwa upande wake Kingunge, amepinga vikali muundo huo akisema utavunja udugu na mshikamano wa Watanzania uliodumu kwa nusu karne. Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliikosoa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuweka kipengele cha muundo wa Serikali tatu.

Kingunge alisema hoja ya Serikali tatu haijatolewa na wananchi kama inavyodaiwa na kwamba anaamini hoja hiyo imesukwa na kuingizwa katika rasimu hiyo na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba, inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

“Mimi siamini hata kidogo eti wazo la kuwa na muundo wa serikali tatu limetolewa na wananchi, si kweli, hili wazo limewekwa na hao walioliweka kwenye rasimu nashangaa umakini wao.

“Rasimu ya Katiba mpya, inapendekezwa kwamba muundo mpya wa Serikali tatu, katika maneno yao wenyewe watu wa tume kuwa bila serikali tatu Muungano utavunjika, jambo la ajabu sana.

“Sisi tuna Muungano wa serikali mbili kwa nusu karne sasa bado unadunda na umeshika nafasi yake katika jumuiya za kimataifa, ni tishio kuwatoa watu huko.

“Wanaodai kwamba jawabu la Muungano bora ni serikali tatu hoja yao kubwa kwamba kuna kero za Muungano ambazo ni nzito kiasi kwamba tunataka aina mpya ya muungano, kuna mambo fulani fulani ambayo hayajibiwi sawa sawa.

Suala la kero ni pana, lakini unapofanya kuwa sababu za kutuondolea udugu uliodumu kwa nusu karne ni kukosa umakini,” alisema Kingunge.
Share on Google Plus

0 comments: