RAYC AOKOKA NAKUBATIZWA KANISA LA SILOAM JIJINI DAR

MSANII wa Kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ameamua kuokoka na kumrudia Mungu na kubatizwa katika Kanisa la Siloam, jijini Dar es Salaam. Ray C alikuwa akipatiwa tiba kutokana na kuathirika na utumiaji wa dawa za kulevya, ikiwa ni msaada kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza jana Dar es Salaam kwa simu, Ray C alisema ameamua kumrudia Mungu na kuachana na mambo ya kidunia kutokana na mengi
kumsibu katika kipindi chote cha ujana wake.

“Nimebatizwa rasmi katika kanisa la Siloam na nalishika neno na kutenda neno katika maisha yangu mapya, shetani hana nafasi tena katika maisha yangu, nimepewa mamlaka na Mungu nimkanyage wala asinizoee kamwee Ameeen,” alisema.
Share on Google Plus

0 comments: