HABARI KAMILI

HABARI KAMILI

Viongozi waliotokwa na machozi hadharani

ImageReutersImageRais Obama ametokwa na machozi hadharani mara kadha
Rais wa Marekani aligonga vichwa vya habari alipotokwa na machozi alipokuwa akiwahimiza Wamarekani wakubali mabadiliko kwenye masharti ya uuzaji wa silaha Marekani Jumanne.
Alizidiwa na hisia alipokuwa akisimulia kuhusu shambulio la ufyatuaji risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook mwaka 2012 ambapo watoto 20 na watu wazima sita.
Hii haikuwa mara yake ya kwanza kutokwa na machozi akizungumzia kisa hicho.

ImageAP
Lakini kiongozi huyu hayuko peke katika kutokwa na machozi hadharani.
Wawafahamu hao wengine?

Machozi ya Olimpiki
ImageGetty
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anajulikana pia kwa kutokwa na machozi hadharani.
Alibubujikwa na machozi mwaka 2009 baada ya mji wa Rio de Janeiro kutangazwa kwamba ungekuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016.
Machozi yake hayakuathiri umaarufu wake na ni mmoja wa marais waliopendwa sana katika historia ya aifa hilo.

Wasiwasi wa Karzai
ImageGetty

Rais wa zamani wa Hamid Karzai aligonga vichwa vya habari duniani alipolia kuhusu hali ya Afghannistan wakati wa kutoa hotuba katika shule ya upili ya Kabul Septemba mwaka 2010.
Alitokwa na machozi alipokuwa akizungumzia mapigano nchini mwake, akisema alikuwa na wasiwasi kwamba hilo lingemfanya mwanawe kutorokea ng’ambo.

Kilio kikao cha wanahabari
ImageGetty Images
Video ya mwanasiasa wa Japan aliyelia baada ya kuulizwa maswali na wanahabari kuhusu matumizi yake ya pesa ilivuma sana mtandaoni Julai 2014.
Ryutaro Nonomura alitokwa na machozi alipotakiwa kujibu madai kwamba alikuwa ametumia pesa za umma kwa safari za kibinafsi.
Alisisitiza kwamba zilikuwa ziara za kikazi.
Baadaye alijiuzulu.

Machozi ya ushindi
ImageAP
Rais wa Urusi Vladimir Putin alionekana kutokwa na machozi alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake Manezhnaya Square, Moscow, baada ya kupata habari kwamba alikuwa ameshinda uchaguzi wa urais Machi 2012.
Machozi yake yalikuwa kinyume kabisa na sifa zake kama mtu mwenye roho ngumu na asiyetekwa na hisia. Baadaye, msemaji wa Putin alisema Putin alikuwa amezidiwa na upepo na baridi na wala si hisia zilizomteka.

Machozi ya kampeni
ImageAFP
Wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais 2008 Hillary Clinton alitokwa na machozi akiwa New Hampshire, alipoulizwa na mwananchi, “Utafanyaje hayo?”
Suti yake ilibadilika na machozi kumtoka alipokuwa akimjibu.
Alifafanua baadaye: "Ningekuwa na wasiwasi sana kujihusu iwapo singekuwa na hisia kwamba hilo lilikuwa muhimu na la maana.”
Waziri huyo wa zaman wa mambo ya nje wa Marekani alitaka urais 2008 lakini akashindwa na Rais Barack Obama mbio za kumsaka mgombea wa chama cha Democratic.

Kuondoka madarakani
ImageGetty Images
Tarehe 28 Novemba 1990, Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Margaret Thatcher alitokwa na machozi alipokuwa akitoa hotuba ya kuaga akiwa amesimama kwenye vidato vya jumba la Downing Street.
Kiongozi huyo wa kwanza mwanamke Uingereza, aliyejulikana kama Iron Lady, aling’atuka baada ya baraza lake la mawaziri kukataa kumuunga mkono uchaguzini.
Alionekana akitokwa na machozi, akipungia watu mikono kutoka kiti cha nyuma cha gari alipokuwa akiondoka afisini mara ya mwisho.

Teknolojia ya video katika kandanda?

Teknolojia ya video huenda ikafanyiwa majaribio msimu ujao katika ligi kuu za kandanda za baadhi ya nchi baada ya uamuzi wa Bodi ya Shirikisho la Kimataifa la Kandanda – IFAB kuijaribu teknolojia hiyo
Maafisa wa kandanda wa Uholanzi na Uingereza ni miongoni mwa mashirikisho yanayosema kuwa matumizi ya mfumo wa kurudishwa nyuma video na kuangalia tena yanaweza kufanyiwa majaribio katika michuano ya ya ndani.
IFAB inapendekeza kuufanyia majaribio mfumo wa kuwasaidia maafisa wa mechi kupitia video katika sehemu muhimu zinazouathiri mchezo kama vile magoli yenye utata na maamuzi ya penalti. Mipango hiyo itapigiwa kura katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa IFAB mwezi Machi.
Katibu wa IFAB Lukas Brud amesema majaribio hayo yataonyesha namna ya kutumia kwa njia nzuri teknolojia ya video – iwe ni kutumiwa au kutoumiwa video pembeni mwa uwanja au ndani ya gari dogo nje ya uwanja na ikiwa mchuano unapaswa kusitishwa kwa muda au la. Majaribio hayo huenda yakafanywa kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu.
Tenkolojia ya video huenda ikawa hatua ya karibuni kuyafanya maisha ya marefarii wa uwanjani kuwa rahisi, miaka mitatu baada ya IFAB kuidhinisha matumizi ya teknolojia ya kuamua kama mpira umevuka mstari wa lango au la ambayo inatumika katika ligi kubwa na mashindano makuu kama vile Kombe la Dunia.

Mtu mmoja afariki baada ya kutumia dawa za majaribio

Mtu  mmoja  amefariki  na  wengine watano  wako  hospitali baada  ya majaribio  ya  dawa  nchini  Ufaransa kwenda kombo.
Waziri  wa  afya  wa  Ufaransa  Marisol Touraine  amesema leo  kuwa  watu  sita  waliojitolea  kufanya  majaribio  hayo walishiriki  kula  dawa  inayotengenezwa  na  maabara  ya ulaya  kaskazini  magharibi  mwa  mji  wa  Rennes.
Kwa  mujibu  wa  vyanzo karibu  na  mkasa huo, dawa  hiyo ni  ya  kutuliza  maumivu yenye Cannabinoids, kiambato kinachopatikana  katika  mmea  wa  bangi.
Chanzo  kingine  kimesema  kampuni  hiyo  inayofanya utafiti  ilikuwa  inafanya  kazi  hiyo  kwa  niaba  ya  kampuni ya  madawa  ya  Ureno ya Bial.
Waziri  wa  afya  wa  Ufaransa  amesema ajali  mbaya imetokea, na  kuongeza  kwamba  majaribio  hayo yamesitishwa na  watu  wote  waliojitokeza  kuyafanya wametakiwa  kurejea  nyumbani.

Seif amtaka Magufuli aongoze rasmi mazungumzo Zanzibar

Chama cha Wananchi (CUF) kimemuomba Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia moja kwa moja mazungumzo ya kusaka suluhisho la mkwamo wa kisheria na kikatiba visiwani Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Serana, jijini Dar es Salaam, mapema leo (Januari 11), Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ametupilia mbali uwezekano wa kurejewa uchaguzi kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kuna kila dalili kuwa Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye anaongoza mazungumzo visiwani Zanzibar hataki kuitisha kikao cha mwisho kupokea tathmini ya vikao nane vilivyokwishafanyika tangu vilipoanza mwanzoni mwa mwezi Februari, na badala yake wasaidizi wake wanaandaa uchaguzi wa marudio kinyume cha sheria, jambo ambalo CUF haiko tayari.
Hoja ya kurudiwa kwa uchaguzi haina uhalali wa kisheria wala kikatiba. Ni jaribio la kuiingiza nchi kwenye machafuko. Ni kitendo cha kujaribu kumpa uhalali Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi kinyume cha sheria. Na hakikubaliki hata siku moja," alisema Maalim Seif kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na vyombo kadhaa vya habari ndani na nje ya Tanzania.
Kupitia mazungumzo hayo, Maalim Seif ambaye amegombea nafasi ya urais wa Zanzibar mara tano mfululizo kuanzia mwaka 1995, alisema uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 ulifanyika katika mazingira ya amani, haki na uhuru zaidi kuliko chaguzi nyengine huko nyuma, jambo ambalo lilisemwa pia na waangalizi wa ndani na wa kimataifa wa uchaguzi huo.
"Katika uchaguzi huo, ambao unakwenda sambamba na wa Muungano, mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia CCM, John Magufuli alipata kura 194, 387 na (Edward) Lowassa (wa Chadema) alipata kura 211,033." Matokeo ya uchaguzi wa Muungano yaliendelea kama kawaida.
Ili kuukwamua mkwamo uliopo, Maalim Seif amemtaka Rais Magufuli kuingilia kati na kuongoza majadiliano hayo, kupitia vikao vya CCM na CUF, kwani mazungumzo ya sasa yameonesha udhaifu wa kimaamuzi.
Mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar ulianza mara tu baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha, kutangaza kuufuta uchaguzi hapo tarehe 28 Oktoba 2015.

Kitabu cha mapenzi kati ya raia Myahudi na Muislamu wa Palestina chaongoza kwa mauzo

Kitabu cha mapenzi kati ya raia Myahudi na mwenzake Muislamu wa Palestina kinaongoza kwa mauzo baada ya wizara ya elimu nchini Israel kukataa kukiorodhesha katika mtaala wa elimu shuleni.

Maafisa walihofia kwamba Borderlife kilichotungwa na Dorit Rabinyan kinaweza kuongeza uhusiano wa kimapenzi kati ya raia wa Kiyahudi na wenzao wa Kiarabu.

Lakini hatua hiyo ilizua hisia kali na kukifanya kitabu hicho kununuliwa na wengi.

Uchapishaji ughaibuni pia unaharakishwa na tafsiri yake inajadiliwa nchini Hungury,Uhispania na Brazil.

Ajenti wa Bi Rabinyan amesema kuwa zaidi ya vitabu 5,000 vimeuzwa katika juma moja pekee,vingi vikiuzwa katika soko la Israel huku maduka mengi yakiwa yamemaliza vitabu hivyo.

Mwigizaji mwenye asili ya Zimbabwe kuigiza mamake mwanamuzi Tupac Shakur.

Mwigizaji mwenye asili ya Zimbabwe, ambaye aliigiza kwenye filamu ya Walking Dead, ameteuliwa kuigiza mamake mwanamuziki mashuhuri Tupac Shakur.

Danai Gurira ambaye alizaliwa 1978 eneo la Grinnell, jimbo la Iowa wazazi wake walipokuwa wanaishi Marekani.

Gurira huigiza kama Michonne katika filamu ya Walking Dead.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari za burudani Deadline, Gurira ndiye aliyeteuliwa kumuigiza Afeni Shakur kwenye filamu kuhusu maisha yake ambayo imepewa jina All Eyez on Me.

Mwelekezi wa filamu hiyo ni Benny Boom.

Mwanagenzi Demetrius Shipp Jr ataigiza kama 2Pac.

Afeni Shakur halisi, ambaye ni mwanaharakati wa zamani wa kisiasa na mfuasi wa chama cha Black Panther, ndiye mwandalizi mkuu wa filamu hiyo.

Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi 1996, akiwa na umri wa miaka 25.

Wazazi wa Gurira, Josephine Gurira na Roger Gurira, walihamia Marekani 1964 lakini wakarejea Zimbabwe baada ya uhuru Desemba 1983.

Baada ya kumaliza masomo ya shule ya upili, Danai Gurira alirejea Marekani na kusomea shahada ya kwanza katika saikolojia chuo cha Macalester, na baadaye akapata shahada ya pili katika sanaa kutoka kitivo cha Tisch, chuo kikuu cha New York.

Msimamo ndoa za jinsia moja makanisa ya Anglikana

Kanisa la Kianglikana duniani limesisitiza kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke na likasimamisha ushirika wa jimbo la Marekani lililotambua ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Jimbo hilo la Marekani, ambalo kwa Kiingereza hujiita Episcopal Church, sasa halitaruhusiwa kushiriki kikamilifu katika masuala ya kanisa hilo.
Viongozi wa kanisa la Kianglikana duniani, waliokutana Canterbury, wamesema kanisa hilo lilikiuka Imani inayofuata na waumini wengi wa kanisa la Kianglikana kuhusu ndoa.
Marufuku hiyo ya muda ambayo imepewa jimbo hilo a Marekani inalenga kuzuia kugawanyika kabisa kwa kanisa hilo kutokana na tofauti kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Ndoa hizo zimekuwa zikipingwa sana na majimbo ya kanisa hilo barani Afrika.
Uamuzi wa kusimamisha uanachama wa jimbo hilo la Marekani ulifanywa katika mkutano ambao umeeleza kuwa "mkali sana".
Askofu wa sasa wa jimbo hilo la Marekani Michael Curry amesema uamuzi huo "utasababisha uchungu mwingi". Mzozo kuhusu ndoa za jinsia moja ulianza kutokota baada ya kutawazwa kwa Kasisi Gene Robinson, aliyekuwa ametangaza hadharani kuwa mpenzi wa jinsia moja, kuwa askofu wa dayosisi ya New Hampshire ya jimbo hilo la Marekani mwaka 2003. Hatua hiyo ilizua mgawanyiko mkubwa miongoni mwa viongozi na waumini wa kanisa hilo duniani.

Hatimaye Lionel Messi achaguliwa mchezaji bora wa mwaka 2015

Ikiwa ni awamu ya tano kwa MCHEZAJI Lionel Messi kutwaa taji hilo ambapo taji la kwanza alitwaa mwaka  2009, mwaka 2010 alifanikiwa kutwaa kwa mara nyingine taji hilo ,2011 akashinda tena nafasi hiyo kwa mara ya tatu na 2012 akashinda tena kwa Mara ya nne na sasa amechukua tena kwa mara ya tano Kama Mchezaji bora duniani kwa mwaka 2015 japokuwa Rolnaldo alikua ndio Mchezaji mwenye magoli mengi kuliko wenzake lakini jopo la  makocha na waandishi pamoja na viongozi wa timu ndio waliomchagua Messi kuwa MCHEZAJI bora. Rinaldo alionekana kwenye hali ya kawaida baada ya kutangazwa kwa Messi kuwa mshindindi wa tuzo hizo huku Neymar pia hakionyesha kupokea matokeo kwenye hali ya kawaida tofauti na ilivyofikiriwa kuwa wangepaniki.

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius aomba kubadilisha kesi mahakamani

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ametuma ombi kwenda kwa mahakama ya kikatiba nchini humo la kutaka aruhusiwe kubadili uamuzi katika kesi ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Mahakama ya rufaa ilibadili hukumu ya awali ya kumuua Bi Steenkamp kutoka kuua bila kukusudia hadi kuua.

Lakini mawakili wake wanasema kuwa mahakama ilifanya makosa. Pistorius anakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 15 ikiwa atashindwa kubadili uamuzi huo wa mahakama ya rufaa.

Choo kinachojisafisha chenyewe pamoja namtumiaji pia.

Kinaitwa CHOO chenye akili kinachofunguka chenyewe unapokikaribia na kujisafisha chenyewe, kimeonyeshwa kwenye maonyesho ya bidhaa za kielectroniki Mjini Las Vegas, Marekani. Kwa mujibu Wa msemaji wa kampuni ya Toto, choo hicho pia kina uwezo Wa kumsafisha mtumiaji kwa kutumia kifaa maalumu kinachotoa maji ya vuguvugu na hewa ya moto anapokuwa amekikalia.
Licha ya kuwa bei yake ni dola 9,800, zaidi ya vyoo milioni 40 tayari vimeuzwa. Mchakato wa choo hicho kujisafisha kutumia mchanganyiko wa dawa za Kusafisha pamoja na kioo maalumu kilichotengenezwa na madini ya Zirconium na Titanium oxide.

CUF: Uchaguzi unaweza kuzua vurugu Zanzibar "Maalim Seif"

Chama cha Wananchi (CUF) kimeonya kuwa kurudiwa kwa uchaguzi visiwani Zanzibar kunaweza kusababisha vurugu na kumtaka Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kuingilia kazi kutatua mzozo ulitokana na uchaguzi visiwani humo.
Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif, akihutubia wanahabari, amesema chama hicho hakitaki uchaguzi urudiwe na kuendelea kusisitiza msimamo wa awali kwamba mshindi wa uchaguzi uliofanywa 25 Oktoba mwaka jana anafaa kutangazwa.
"Ni vyema tukaweka waziwazi hapa kwamba kurudiwa uchaguzi sio suluhishona hakukubaliki. Kwani, kama nilivyoonesha hakuna hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi kurudiwa," amesema Bw Seif.
Bw Maalim Seif, aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho, alionekana kupendekeza mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha ang’atuke.
Rais wa Zanzibar aongezewa muda
Matokeo ya uchaguzi Zanzibar yafutwa
Chama hicho kimemtuhumu Rais wa visiwani Mohamed Ali Shein wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kukwamisha mashauriano ya kutafuta suluhu ili ZEC itangaze marudio ya uchaguzi.
Ingawa tarehe kamili haijatangazwa, Bw Seif na wenzake wamedokeza kwamba huenda kukawa na mipango ya kuitisha marudi ya uchaguzi tarehe 28 Februari 2016.
CCM imeonekana kuunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi visiwani na majuzi viongozi wa chama hicho waliwataka wafuasi wake visiwani kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tangazo hilo lilishutumiwa vikali na viongozi wa CUF.

Nani mshindi kwenye tuzo za Ballon d' Or,... Messi, Ronaldo au Neymar

Mmoja kati ya miyamba ya soka duniani,Lionel Messi,Christiano Ronaldo au Neymar huenda akatawazwa kuwa mshindi wa tuzo la Ballon d'Or,tuzo linalopewa mchezaji bora duniani.
Tuzo hiyo inayopigiwa kura na makocha wa kimataifa ,manahodha wa timu na waandishi litalowewa kwa mara ya 60 katika hafla ya kipekee mjini Zurich nchini Switzerland.
Kutoka Stanley Matthews aliyeshinda mwaka tuzo hilo mwaka 1956 hadi Christiano Ronaldo mwaka uliopita,washindi wake wameorodheshwa katika kipindi cha miaka 59 iliopita.
Katika miaka ya kombe la dunia asilimia 47 ya washindi wa tuzo hilo waliyasaidia mataifa yao kushinda kombe hilo ikiwemo Bobby Charlton mwaka 1966,Mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane mwaka 1998 pamoja na nahodha wa timu ya Itali Fabio Cannavaro mwaka 2006.
Ni Asilimia 36 pekee waliosaidia mataifa yao kushinda kombe la bara Ulaya.

Mgawanyiko wanukia makanisa ya kiangliakana

Mgawanyiko katika kanisa la Kianglikana kuhusu suala la mapenzi ya jinsia moja halitakuwa janga bali itakuwa ni kufeli. Hii ni kwa mujibu wa askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby.
Akizungumza kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa kanisa hilo Welby, anasema kuwa anataka kuwepo uwiano lakini hiyo ina maana ya kupata njia za kutofautiana kwa nja iliyo nzuri.
Kanisa la kianglikana lina waumini karibu millioni 80 kote duniani katika zaidi ya nchi 160, wengi wakiwa wanamuona askofu Welby kama uongozi wa kanisa hio.
Watunza sera wanasema kuwa kanisa la kianglikana ni lazima lishikilie tamaduni zake.
Lakini maoni ya nchi nyingi za Afrika ambapo mapenzi ya jinsia moja ni makosa, hufanya mambo kuwa magumu kwa kanisa hilo kuwa na msimamo mmoja, huku makanisa mengi yakipinga vikali ndoa za jinsia moja na mskofu shoga.
Kuna wasi wasi kuwa waakilishi kutoka nchi za Afrika huenda wakaondoka kwenye mkutano wa Canterbury.

Raia wa India atengeneza gari kubwa duniani


Image caption
Gari kubwa dunianiMchoraji wa miundo ya magari nchini India Sudhakr Yadav amejaribu kuweka rekodi ya pili ya Guiness kwa kutengeneza gari analotumai litakuwa ndilo kubwa zaidi duniani.
Gari hilo, ambalo limeundwa likifanana na gari aina ya Ford Toure lililoundwa mwaka 1922, lina urefu wa futi 26 (mita 8) kwenda juu na ukubwa wa futi 50 lina ukubwa maradufu wa basi lililo na ghorofa mbili mjini London.
Bwana Yadav tayari anashikilia rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuwa na baiskeli ndefu zaidi duniani.
Mchoraji huyo wa miundo ya magari anamiliki makavazi ya magari katika mji wa Hyderabad ulioko kusini mwa India ambapo anaonyesha mitindo tofauti ya magari
Magari hayo yana maumbo na ukubwa tofauti .
''Tunalenga kuvunja rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuunda gari kubwa duniani. Ni rekodi mpya na nina matumaini nitaipata," alisema.
Anatarajia gari hilo liwe na mngurumo sawa na wa magari ya mbio za langalanga au Formula One.
Baiskeli yake ya magurudumu matatu ni ndefu zaidi ya gari hilo ikiwa na futi 41.5 kwenda juu.

Raia wa Cameroon Hayatou kuongoza Fifa kwa muda

Issa HayatouImage copyrightAFP

Image caption
Hayatou ndiye makamu wa rais wa Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi kwa sasaKiongozi wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho la soka duniani Fifa kwa muda.
Hayatou atachukua usukani kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais wa Fifa Sepp Blatter kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo, shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema kupitia taarifa.
Hayatou, aliyeongoza CAF tangu 1988, atachukua usukani kwa mujibu wa sheria za Fifa, akiwa ndiye makamu wa rais katika kamati tendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.
Baadaye, Hayatou ametoa taarifa na kusema amepokea majukumu hayo mapya lakini ataongoza tu kwa muda.
“Rais mpya atachaguliwa kwenye Mkutano Mkuu Februari 26, 2016. Na mimi mwenyewe sitawania,” amesema kupitia taarifa.
“Hadi mkutano huo ufanyike, naahidi kwamba nitajitolea kwa nguvu zangu zote kutumikia shirikisho hili, mashirikisho wanachama, waajiri wetu, washirika na mashabiki wa soka popote walipo.”
Aidha, ameahidi kuendelea kushirikiana na watawala na kuendeleza uchunguzi kwenye shirikisho hilo lililoyumbishwa na madai ya ulaji rushwa.

Raia wa nchini China wakamatwa nchini Tanzania wakishukiwa kwa usafirishaji wa Pembe za ndovu

Image captionUWINDAJI HARAMU: STORY BY HABARI KAMILI
Jopo maalum la wanyama pori nchini Tanzania limewakamata baadhi ya raia wa Uchina wanaoushukiwa kusafirisha pembe za ndovu.
Makundi ya kampeni dhidi ya uwindaji haramu yanasema kuwa wale waliokamatwa ni pamoja na mwanamke aliyepewa jina la utani 'Malkia wa pembe za ndovu' {Yang Feng Glan}.
Wahifadhi wameitaja Tanzania kama shina la uwindaji haramu wa pembe za ndovu ,na kuongezea kuwa ndovu 8,500 waliuawa katika kipindi cha miaka mitano iliopita.

DC Makonda...sitasahau niligombea chakula cha mbwa...

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
MAISHA usiyapimie! Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema katika harakati zake za maisha, aliwahi kugombea chakula na mbwa wakati akiwa chuoni wilayani Bagamoyo, kitu ambacho kilimuumiza mno.
Makonda alitoa maneno hayo wakati akizungumza katika semina ya kujikomboa kutoka katika umasikini inayofanyika kila Jumapili katika Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Makumbusho jijini Dar es Salaam ambayo mhamasishaji mahiri nchini, Eric Shigongo hushiriki.
“Mama yangu alikopa Finca, hela hazikutosha ada, vitu vyake vyote vya ndani vikachukuliwa, chuoni nilikuwa nasubiri wenzangu wakishakula kantini, nawahi kula makombo kabla watu waliotoa oda ya chakula cha mbwa hawajaja. Wakati mwingine nililazimika kugombana na watu waliokuja kuwachukulia hao mbwa kama tukikutana.
“Siku moja Bi. Mkubwa alikuja shuleni na mzigo wa unga bila mboga, hakuwa na chochote na wala mimi sikuwa na fedha. Nilifanya bidii kwenye masomo hatimaye leo hii mimi ni mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kama mimi nilitokea huko na niko hapa leo, ni wazi kuwa hata nyinyi mnaweza kubadilika na kuwa watu wengine kabisa katika maisha,” alisema Makonda, mmoja wa vijana wengi waliopewa nafasi za juu za uongozi na serikali ya awamu ya nne.
Kwa simulizi zaidi ya Paul Makonda, usikose kufuatilia magazeti ya Global Publishers.

Manchester City inamtaka Raheem Sterling?

sterling
Klabu ya Manchester City imetuma ofa ya paundi milioni 40 kwenda kwa klabu yaLiverpool kwa ajili ya kumnunua kiungo mshambuliaji raia wa England, Raheem Sterling.
Ofa hii inakuwa ya pili toka kwa City ambao wanaonekana kuwa wamepania katika azma yao ya kumsajili kiungo huyu ambaye ametokea kuwa moja kati ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Liverpool na timu ya taifa ya England katika siku za hivi karibuni.
Taarifa hii inakuwa sehemu nyingine katika mfululizo wa ‘filamu’ inayoendelea kati yaRaheem Sterling na Liverpool baada ya kiungo huyo kuweka wazi kuwa amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo inayomilikiwa na Wamarekani, Fenway Sports Group.
Awali kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita Sterling alifanya mazungumzo yaliyorekodiwa na kituo cha BBC ambapo alifichua kuwa amegoma kusaini mkataba mpya baada ya kutoridhishwa nao huku akionekana wazi kuwa amejiandaa kuondoka.
Liverpool imesema kuwa haitasikiliza ofa yoyote iliyoko chini ya oaundi milioni 50 ambayo wanaona ndio thamani halisi ya Raheem Sterling.
Liverpool imesema kuwa haitasikiliza ofa yoyote iliyoko chini ya paundi milioni 50 ambayo wanaona ndio thamani halisi ya Raheem Sterling.
Wakala wa mchezaji huyo naye hakusita kuweka wazi kuwa mteja wake atajiunga na moja kati ya wapinzani wakubwa wa Liverpool ambapo awali ilivumishwa kuwa Manchester United na Manchester City zingeingia vitani kusaka saini yake.
Manchester City hawakuchelewa ambapo haraka waliingia sokoni na kupeleka ofa ya paundi milioni 30 ambayo Liverpool iliikataa kabla ya kuja na ofa ya pili ambayo kama ya kwanza pia imekataliwa.
Liverpool wameweka wazi kuwa hawatasikiliza ofa yoyote ambayo iko chini ya paundi milioni 50 ambazo wao kama klabu wameweka kama thamani ya mchezaji huyo.

Hali si shwari ndani ya FIFA, kashfa zazidi kufichuliwa !!

0D62059700000514-0-Russia_and_Qatar_are_the_respective_hosts_of_the_2018_and_2022_W-m-7_1434533375341
Wapelelezi wanaofatilia kashfa ya rushwa inayohusu shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wameahidi kufichua makubwa zaidi baada ya kugundua siri nzito zilizojificha kwenye mchakato wa kuchagua mwenyeji wa kombe la dunia.
Wapepelezi hao wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Uswisi, Michael Lauberwamesema kuwa kuna matukio karibu 53 ya uchakachuzi na utakatishaji haramu wa fedha ambayo yamegundulika kwenye michakato tofauti ya kumpata mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia na matukio haya yamehusishaa watu wazito ambao kama yatagundulika undani wake yatazua hofu na utata mkubwa.
Mwanasheria mkuu nchini Uswissi Michel Lauber akizungumza na waandishi wa habari.
Mwanasheria mkuu nchini Uswissi Michael Lauber.
Mwanasheria huyo ameonya kuwa hatajali kama upelelezi wake utasababisha hasara ya fedha  au kupokonywa uwenyeji kwa nchi za Urusi na Qatar na anachojali ni ufanisi wa kazi yake na si kitu kingine.
Imedaiwa kuwa upelelezi huu unahusisha kuhojiwa kwa viongozi wa juu wa FIFA akiwemo rais wa zamani Sepp Blatter ambaye hivi karibuni alitangaza kujiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha tano.
Rais wa Fifa wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .
Rais wa FIFA wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .
Viongozi kadhaa wa zamani wa FIFA wakiwemo Mmarekani, Chuck Blazer na rais wa zamani wa chama cha soka cha Trinidad and Tobago, Jack Warner wameahidi kutoa ushirikiano kwa wapelelezi huku wakiahidi kuwa watazungumza bila kuficha.

Hii ndio ahadi ya kuvua nguo mbele ya camera baada ya ushindi wa Timu yake..

Kila shabiki huwa na hisia zake pindi timu anayoipenda inapokua ikicheza na mara nyingi tumeshuhudia watu wakitoa hadi mbalimbali endapo timu yake itaibuka na ushindi ama la.
Kuna hii stori  ya mtangazaji wa habari za michezo huko Venezuela imenifikia mtu wangu,,yeye aliwaahidi mashabiki kuwa endapo timu yake ya Venezuela itaibuka na ushindi basi atavua nguo zake mbele ya camera.Sasa baada ya mchezo kumalizika kati ya Venezuela ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Colombia katika mashindano ya Copa America yanayoendelea, mtangazaji huyo alitimiza ahadi yake ya kuvua nguo mbele ya camera wakati akitangaza.

Ratiba ligi kuu ya England msimu ujao yote iko hapa

fixx
Ratiba ya ligi kuu ya England tayari imetoka rasmi ambapo mabingwa wa ligi hiyo, Klabu ya Chelsea itaanza kutetea taji la ligi hiyo wakati itakapoikaribisha nyumbani Swansea siku ya August 8 2015.
Manchester City iliyomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itafunga safari kupambana na West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na vigogo wa Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.
Arsenal itaialika West Ham, huku Liverpool ikiivaa Stoke CityNewcastle itakabiliana naSouthampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
RATIBA KAMILI YA LIGI KUU YA ENGLAND MSIMU WA 2015-2016 hii hapa.
Agosti 8
Bournemouth v Aston Villa
Arsenal v West Ham United
Chelsea v Swansea City
Everton v Watford
Leicester City v Sunderland
Manchester United v Tottenham Hotspur
Newcastle United v Southampton
Norwich City v Crystal Palace
Stoke City v Liverpool
West Bromwich Albion v Manchester City
Agosti 15
Aston Villa v Manchester United
Crystal Palace v Arsenal
Liverpool v Bournemouth
Manchester City v Chelsea
Southampton v Everton
Sunderland v Norwich City
Swansea City v Newcastle United
Tottenham Hotspur v Stoke City
Watford v West Bromwich Albion
West Ham United v Leicester City
Agosti 22
Arsenal v Liverpool
Crystal Palace v Aston Villa
Everton v Manchester City
Leicester City v Tottenham Hotspur
Manchester United v Newcastle United
Norwich City v Stoke City
Sunderland v Swansea City
Watford v Southampton
West Bromwich Albion v Chelsea
West Ham United v Bournemouth
Agosti 29
Bournemouth v Leicester City
Aston Villa v Sunderland
Chelsea v Crystal Palace
Liverpool v West Ham United
Manchester City v Watford
Newcastle United v Arsenal
Southampton v Norwich City
Stoke City v West Bromwich Albion
Swansea City v Manchester United
Tottenham Hotspur v Everton
 
Septemba 12
Arsenal v Stoke City
Crystal Palace v Manchester City
Everton v Chelsea
Leicester City v Aston Villa
Manchester United v Liverpool
Norwich City v Bournemouth
Sunderland v Tottenham Hotspur
Watford v Swansea City
West Bromwich Albion v Southampton
West Ham United v Newcastle United
 
Septemba 19
Bournemouth v Sunderland
Aston Villa v West Bromwich Albion
Chelsea v Arsenal
Liverpool v Norwich City
Manchester City v West Ham United
Newcastle United v Watford
Southampton v Manchester United
Stoke City v Leicester City
Swansea City v Everton
Tottenham Hotspur v Crystal Palace
 
Septemba 26
Leicester City v Arsenal
Liverpool v Aston Villa
Manchester United v Sunderland
Newcastle United v Chelsea
Southampton v Swansea City
Stoke City v Bournemouth
Tottenham Hotspur v Manchester City
Watford v Crystal Palace
West Bromwich Albion v Everton
West Ham United v Norwich City
 
Oktoba 3
Bournemouth v Watford
Arsenal v Manchester United
Aston Villa v Stoke City
Chelsea v Southampton
Crystal Palace v West Bromwich Albion
Everton v Liverpool
Manchester City v Newcastle United
Norwich City v Leicester City
Sunderland v West Ham United
Swansea City v Tottenham Hotspur
 
Oktoba 17
Chelsea v Aston Villa
Crystal Palace v West Ham United
Everton v Manchester United
Manchester City v Bournemouth
Newcastle United v Norwich City
Southampton v Leicester City
Swansea City v Stoke City
Tottenham Hotspur v Liverpool
Watford v Arsenal
West Bromwich Albion v Sunderland
 
Oktoba 24
Bournemouth v Tottenham Hotspur
Arsenal v Everton
Aston Villa v Swansea City
Leicester City v Crystal Palace
Liverpool v Southampton
Manchester United v Manchester City
Norwich City v West Bromwich Albion
Stoke City v Watford
Sunderland v Newcastle United
West Ham United v Chelsea
 
Oktoba 31
Chelsea v Liverpool
Crystal Palace v Manchester United
Everton v Sunderland
Manchester City v Norwich City
Newcastle United v Stoke City
Southampton v Bournemouth
Swansea City v Arsenal
Tottenham Hotspur v Aston Villa
Watford v West Ham United
West Bromwich Albion v Leicester City
 
Novemba 7
Bournemouth v Newcastle United
Arsenal v Tottenham Hotspur
Aston Villa v Manchester City
Leicester City v Watford
Liverpool v Crystal Palace
Manchester United v West Bromwich Albion
Norwich City v Swansea City
Stoke City v Chelsea
Sunderland v Southampton
West Ham United v Everton
 
Novemba 21
Chelsea v Norwich City
Crystal Palace v Sunderland
Everton v Aston Villa
Manchester City v Liverpool
Newcastle United v Leicester City
Southampton v Stoke City
Swansea City v Bournemouth
Tottenham Hotspur v West Ham United
Watford v Manchester United
West Bromwich Albion v Arsenal
 
Novemba 28
Bournemouth v Everton
Aston Villa v Watford
Crystal Palace v Newcastle United
Leicester City v Manchester United
Liverpool v Swansea City
Manchester City v Southampton
Norwich City v Arsenal
Sunderland v Stoke City
Tottenham Hotspur v Chelsea
West Ham United v West Bromwich Albion
 
Desemba 5 
Arsenal v Sunderland
Chelsea v Bournemouth
Everton v Crystal Palace
Manchester United v West Ham United
Newcastle United v Liverpool
Southampton v Aston Villa
Stoke City v Manchester City
Swansea City v Leicester City
Watford v Norwich City
West Bromwich Albion v Tottenham Hotspur
 
Desemba 12
Bournemouth v Manchester United
Aston Villa v Arsenal
Crystal Palace v Southampton
Leicester City v Chelsea
Liverpool v West Bromwich Albion
Manchester City v Swansea City
Norwich City v Everton
Sunderland v Watford
Tottenham Hotspur v Newcastle United
West Ham United v Stoke City
 
Desemba 19
Arsenal v Manchester City
Chelsea v Sunderland
Everton v Leicester City
Manchester United v Norwich City
Newcastle United v Aston Villa
Southampton v Tottenham Hotspur
Stoke City v Crystal Palace
Swansea City v West Ham United
Watford v Liverpool
West Bromwich Albion v Bournemouth
 
Desemba 26 
A.F.C. Bournemouth v Crystal Palace
Aston Villa v West Ham United
Chelsea v Watford
Liverpool v Leicester City
Manchester City v Sunderland
Newcastle United v Everton
Southampton v Arsenal
Stoke City v Manchester United
Swansea City v West Bromwich Albion
Tottenham Hotspur v Norwich City
 
Desemba 28 
Arsenal v Bournemouth
Crystal Palace v Swansea City
Everton v Stoke City
Leicester City v Manchester City
Manchester United v Chelsea
Norwich City v Aston Villa
Sunderland v Liverpool
Watford v Tottenham Hotspur
West Bromwich Albion v Newcastle United
West Ham United v Southampton
 
Januari 2
Arsenal v Newcastle United
Crystal Palace v Chelsea
Everton v Tottenham Hotspur
Leicester City v Bournemouth
Manchester United v Swansea City
Norwich City v Southampton
Sunderland v Aston Villa
Watford v Manchester City
West Bromwich Albion v Stoke City
West Ham United v Liverpool
 
Januari 12
Bournemouth v West Ham United
Aston Villa v Crystal Palace
Liverpool v Arsenal
Swansea City v Sunderland
 
Januari 13
Chelsea v West Bromwich Albion
Manchester City v Everton
Newcastle United v Manchester United
Southampton v Watford
Stoke City v Norwich City
Tottenham Hotspur v Leicester City
 
Januari 16 
Bournemouth v Norwich City
Aston Villa v Leicester City
Chelsea v Everton
Liverpool v Manchester United
Manchester City v Crystal Palace
Newcastle United v West Ham United
Southampton v West Bromwich Albion
Stoke City v Arsenal
Swansea City v Watford
Tottenham Hotspur v Sunderland
 
Januari 23 
Arsenal v Chelsea
Crystal Palace v Tottenham Hotspur
Everton v Swansea City
Leicester City v Stoke City
Manchester United v Southampton
Norwich City v Liverpool
Sunderland v Bournemouth
Watford v Newcastle United
West Bromwich Albion v Aston Villa
West Ham United v Manchester City
 
Februari 2
Arsenal v Southampton
Crystal Palace v Bournemouth
Leicester City v Liverpool
Manchester United v Stoke City
Norwich City v Tottenham Hotspur
Sunderland v Manchester City
Watford v Chelsea
West Bromwich Albion v Swansea City
West Ham United v Aston Villa
 
Februari 3 
Everton v Newcastle United
 
Februari 6 
Bournemouth v Arsenal
Aston Villa v Norwich City
Chelsea v Manchester United
Liverpool v Sunderland
Manchester City v Leicester City
Newcastle United v West Bromwich Albion
Southampton v West Ham United
Stoke City v Everton
Swansea City v Crystal Palace
Tottenham Hotspur v Watford
 
Februari 13 
Bournemouth v Stoke City
Arsenal v Leicester City
Aston Villa v Liverpool
Chelsea v Newcastle United
Crystal Palace v Watford
Everton v West Bromwich Albion
Manchester City v Tottenham Hotspur
Norwich City v West Ham United
Sunderland v Manchester United
Swansea City v Southampton
 
Februari 27 
Leicester City v Norwich City
Liverpool v Everton
Manchester United v Arsenal
Newcastle United v Manchester City
Southampton v Chelsea
Stoke City v Aston Villa
Tottenham Hotspur v Swansea City
Watford v Bournemouth
West Bromwich Albion v Crystal Palace
West Ham United v Sunderland
 
Machi 1 
Bournemouth v Southampton
Arsenal v Swansea City
Aston Villa v Everton
Leicester City v West Bromwich Albion
Liverpool v Manchester City
Manchester United v Watford
Norwich City v Chelsea
Sunderland v Crystal Palace
West Ham United v Tottenham Hotspur
 
Machi 2 
Stoke City v Newcastle United
 
Machi 5 
Chelsea v Stoke City
Crystal Palace v Liverpool
Everton v West Ham United
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Bournemouth
Southampton v Sunderland
Swansea City v Norwich City
Tottenham Hotspur v Arsenal
Watford v Leicester City
West Bromwich Albion v Manchester United
 
Machi 12 
Bournemouth v Swansea City
Arsenal v West Bromwich Albion
Aston Villa v Tottenham Hotspur
Leicester City v Newcastle United
Liverpool v Chelsea
Manchester United v Crystal Palace
Norwich City v Manchester City
Stoke City v Southampton
Sunderland v Everton
West Ham United v Watford
 
Machi 19 
Chelsea v West Ham United
Crystal Palace v Leicester City
Everton v Arsenal
Manchester City v Manchester United
Newcastle United v Sunderland
Southampton v Liverpool
Swansea City v Aston Villa
Tottenham Hotspur v Bournemouth
Watford v Stoke City
West Bromwich Albion v Norwich City
 
Aprili 2 
Bournemouth v Manchester City
Arsenal v Watford
Aston Villa v Chelsea
Leicester City v Southampton
Liverpool v Tottenham Hotspur
Manchester United v Everton
Norwich City v Newcastle United
Stoke City v Swansea City
Sunderland v West Bromwich Albion
West Ham United v Crystal Palace
 
Aprili 9 
Aston Villa v Bournemouth
Crystal Palace v Norwich City
Liverpool v Stoke City
Manchester City v West Bromwich Albion
Southampton v Newcastle United
Sunderland v Leicester City
Swansea City v Chelsea
Tottenham Hotspur v Manchester United
Watford v Everton
West Ham United v Arsenal
 
Aprili 16 
Bournemouth v Liverpool
Arsenal v Crystal Palace
Chelsea v Manchester City
Everton v Southampton
Leicester City v West Ham United
Manchester United v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Norwich City v Sunderland
Stoke City v Tottenham Hotspur
West Bromwich Albion v Watford
 
Aprili 23 
Bournemouth v Chelsea
Aston Villa v Southampton
Crystal Palace v Everton
Leicester City v Swansea City
Liverpool v Newcastle United
Manchester City v Stoke City
Norwich City v Watford
Sunderland v Arsenal
Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion
West Ham United v Manchester United
 
Aprili 30 
Arsenal v Norwich City
Chelsea v Tottenham Hotspur
Everton v Bournemouth
Manchester United v Leicester City
Newcastle United v Crystal Palace
Southampton v Manchester City
Stoke City v Sunderland
Swansea City v Liverpool
Watford v Aston Villa
West Bromwich Albion v West Ham United
 
Mei 7
Bournemouth v West Bromwich Albion
Aston Villa v Newcastle United
Crystal Palace v Stoke City
Leicester City v Everton
Liverpool v Watford
Manchester City v Arsenal
Norwich City v Manchester United
Sunderland v Chelsea
Tottenham Hotspur v Southampton
West Ham United v Swansea City
 
Mei 15 
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Leicester City
Everton v Norwich City
Manchester United v Bournemouth
Newcastle United v Tottenham Hotspur
Southampton v Crystal Palace
Stoke City v West Ham United
Swansea City v Manchester City
Watford v Sunderland
West Bromwich Albion v Liverpool