SUGU: SERIKALI IUNDE TUME YA KUSAIDIA WASANII WA TANZANIA

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', ameitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza mapato ya wasanii yanayoibiwa na kampuni za simu nchini,
kutokana na kutumia nyimbo zao kama miito ya simu.

Akiuliza swali bungeni jana mkoani Dodoma, Mbilinyi alisema mbali na wasanii hao kudhulumiwa fedha zao, lakini pia Serikali inapoteza mamilioni ya mapato kutokana na biashara hiyo inayofanywa na kampuni za simu nchini.

Alisema ni udhaifu kwa Serikali kusema hawana taarifa za mapato, ambayo kampuni za simu zinayapata kutokana na kutumia miito ya simu ya nyimbo za wasanii, kampuni hizo inazo taarifa, lakini inazificha kwa makusudi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema ni kweli wasanii wamekuwa wakilalamika kuibiwa mapato ya nyimbo zinazotumiwa na kampuni hizo kama miito ya simu.

“Wazo la kuunda tume huru tumelichukua tutalifanyia kazi, lakini kwa kuwa Mbunge na yeye ni msanii, tushirikiane kuhakikisha tunadhibiti wizi wa kazi za wasanii,” alisema Makamba.
Share on Google Plus

0 comments: