''TUNATAKA SERIKALI MBILI'' WAKUU WA MKOA NA WALIYA

WAKUU wa mikoa na wilaya nchini, jana waliungana na wananchi wengine kutoa maoni kwa ajili ya kuboresha rasimu ya Katiba mpya. Katika maoni yao, viongozi hao wa mikoa na wilaya walipendekeza Katiba mpya iweke muundo wa serikali mbili kwa madai kuwa muundo huo utasaidia kulinda Muungano.

Viongozi hao walisema muundo mwingine tofauti na serikali mbili ni hatari na kwamba muundo wa serikali tatu haufai, kwani unaweka mwanya wa Muungano kuvunjika.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa jopo hilo, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema huo ndiyo msimamo wa baraza lao.

Kandoro alisema baraza lao limejikita zaidi kujadili masuala muhimu na kueleza kuwa wamepandekeza mambo manne kwa lengo la kuiboresha rasimu hiyo.

“Rasimu ya Katiba imetoa mfumo wake utakuwa na shirikisho linaloundwa na serikali Tatu ‘Ibara 57(1) yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.

“Sababu zetu za msingi kwa mgawanyiko wa nchi yetu ilivyo, kuna kila dalili ya rasilimali zinazotegemewa kuendesha kwa kiasi kikubwa serikali zote tatu zinazopendekezwa kuuweka Muungano huo katika hali tete,” alisema.

“Pia tumependekeza masuala ya kisheria, Katiba kama sheria mama iundwe kwa lengo la kutoa matamko ya msingi ya haki na wajibu wa wananchi, viongozi na
vyombo mbalimbali.

Alisema katika rasimu kuna kipengele kinachoonesha mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 akikutwa mpakani na wazazi wake hawajulikani atakuwa raia wa Tanzani kwa kuzaliwa.

“Kuna wazazi wengine wanaweza wakawaleta watoto wao mipakani na kuwaacha na kuwa raia, mwishowe anaweza kuja kugombea urais, hapa kuna hatari ya kupata rais asiyeraia.

“Kwa hiyo masuala kama ya uraia yanayowagusa wananchi moja kwa moja na rasilimali zao inashauriwa, katiba itoe maelekezo ya wazi ili Mtanzania awe ni mtu anayejipambanua kwa sifa za wazi, badala ya sifa zinazopendekezwa sasa ambazo zinaonekana huko mbele kusababisha utata katika maeneo,” alisema Kandoro.
Share on Google Plus

0 comments: