NYOTA wa Brazil, Neymar ameshinda taji
lake la kwanza Barcelona kufuatia vigogo hao wa Katalunya kutwaa taji la
nne la Super Cup ya Hispania ndani ya miaka mitano kwa faida ya bao la
ugenini, baada ya sare bila kufungana 0-0 usiku wa jana Uwanja wa Nou
Camp.
Baada ya sare ya 1-1 wiki iliyopita
Uwanja wa Calderon, bao la Barca likifungwa na Neymar, aliyetokea benchi
kuisawazishia timu hiyo mjini Madrid, alianzishwa katika kikosi cha
kwanza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo majira haya ya joto
akitokea Santos ya kwao.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi
pia alirejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi, lakini wote walishindwa
kutikisa nyavu za wageni.
Messi alikosa hadi penalti baada ya kugongesha mwamba na mpira ukarejea uwanjani.
Katika mchezo huo, wachezaji wawili
walitolewa nje kwa kadi nyekundu, Filipe Kasmirski dakika ya 80 na Arda
Turan dakika ya 90 na ushei.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Victor
Valdes, Dani Alves, Gerard Pique, Javier Mascherano, Jordi Alba, Sergio
Busquets, Xavi, Cesc Fabregas/Andres Iniesta dk73, Alexis Sanchez/Pedro
dk65, Neymar na Lionel Messi.Atletico Madrid: Thibaut
Courtois, Miranda, Diego Godin, Luis Filipe, Juanfran, Gabi, Koke/Leo
Baptistao dk89, Mario Suarez, Arda Turan/Adrian dk72, Diego Costa, David
Villa/Cristian Rodriguez dk84.
Sema chiiiiizz: Neymar (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake, Dani Alves na Super Cup ya Hispania
Mabingwa: Barcelona wamesherehekea rekodi ya kutwaa Super Cup ya 11 Hispania dhidi ya Atletico Madrid
Mchuano: Lionel Messi (kulia) akipambana na David Villa
Juanfran wa Atletico Madrid (kushoto) akigombea mpira wa juu na Neymar wa Barcelona (kulia)
Anapaa: Cesc Fabregas akiwatoka Joao Miranda na Mario Suarez (kulia)
Mchezaji mwenzake wa zamani: Gerard Pique (kulia) akipambana na mshambuliaji wa Atletico, David Villa
Bao la wazi: Nyota wa Barcelona, Neymar akisikitika baada ya kukosa bao
Anavuta jezi: Arda Turan wa Atletico akimvuta jezi Messi
0 comments: