"NACHEZA POPOTE PALE UWANJANI" MRISHO NGASA

  Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema yuko tayari kucheza kokote atakapopangwa na kocha wake Hans Pluijm.
Kauli hiyo ya Ngassa imekuja siku chache baada ya Mdachi huyo kumchezesha namba 8 wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
.
Akizungumza na gazeti hili, Ngassa alisema kuwa nafasi asiyoweza kuicheza ndani ni ya kipa pekee ambayo ni ngumu na hajawahi kuicheza tangu aanze kucheza soka la ushindani katika mechi mbalimbali.
Ngassa alisema, hachagui nafasi ya kucheza ndani ya uwanja atakayopangwa na kocha wake kutokana na uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi zote akiwa uwanjani.
Aliongeza kuwa, yupo tayari kuendelea kucheza nafasi hiyo namba 8 katika kikosi hicho na kuondolewa namba 7, 9, 10 na 11 ambazo zimezoeleka ndiyo anazozimudu kuzicheza.
“Mimi nina uwezo wa kucheza nafasi zote ndani ya uwanja, nafasi nisiyoweza kuicheza ni kipa pekee, sijawahi kuicheza tangu nianze kujiingiza kwenye soka la ushindani.
“Lakini hizo namba nyingine zote nimezicheza na ndiyo maana kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting nilicheza kwa kiwangocha juu kwa kufunga mabao na kutengeneza pasi nyingi zilizozaa mabao,”alisema Ngassa.
Share on Google Plus

0 comments: