Wakati miili ya wapiganaji hao ikiletwa, tayari familia zao zimeshawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapokea marehemu hao kwa maziko katika maeneo yaliyopangwa na wengine wakisubiri katika mikoa yao.
Dar/mikoani. Wakati miili ya askari wa Tanzania waliokufa Darfur
ikitarajiwa kuletwa keshokutwa, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu
wameanza kuwasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuipokea.
Msemaji wa Mpango wa Kulinda Amani wa Umoja wa
Mataifa na Afrika (UNAMID), kwenye Mji wa Darfur, Chris Cycmakick
alisema jana kuwa miili hiyo ilikuwa ikiendelea
kufanyiwa uchunguzi ambao unatarajiwa kukamilika leo.
kufanyiwa uchunguzi ambao unatarajiwa kukamilika leo.
“Hata kama uchunguzi ukikamilika kesho (leo),
hatuwezi kusafirisha keshokutwa (kesho Ijumaa) kwa kuwa hapa Sudan ni
kama siku ya mapumziko. Sasa utaratibu unafanyika kuisafirisha Jumamosi
kwa ndege ya Umoja wa Mataifa,” alisema Cycmakick.
Wapiganaji hao saba waliuawa na moja ya vikundi
vya waasi walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kulinda amani kupitia
UNAMID huko Darfur.
Uchunguzi wa gazeti hili, ulibaini kuwa wanajeshi
hao wanatoka vikosi vya 42KJ Chabruma, Songea, 44KJ Mbeya, 36KJ
Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea
na Makao Makuu ya Jeshi- Upanga, Dar es Salaam.
Familia zawasili Dar
Wakati miili ya wapiganaji hao ikiletwa, tayari
familia zao zimeshawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapokea marehemu
hao kwa maziko katika maeneo yaliyopangwa na wengine wakisubiri katika
mikoa yao.
Akizungumza na mwandishi wetu jana eneo la Mji
Mpya, Songea, Mama wa marehemu, Rodney Ndunguru, Lucy alisema
wanachosubiri ni kupokea mwili wa marehemu watakapoletewa na jeshi
kutoka Dar es Salaam.
Alisema mwili wa mtoto wake huyo aliyekuwa Kambi
ya 92KJ, Ngerengere mkoani Morogoro utasindikizwa na mke wa marehemu,
Fatma Hajj Ammen anayetokea Zanzibar alikokwenda kujifungua mtoto ambaye
sasa ana miezi minne.Mama huyo alisema kuwa mwanawe huyo kifungua mimba
na aliyekuwa katika kikosi cha makomandoo, atazikwa alikolala baba
yake, eneo la Myangayanga, Songea.
Naye Maria Chaula, mke wa Koplo Oswald Chaula
aliyekuwa Kikosi cha Mizinga katika Kambi ya Chabruma, aliondoka jana
alfajiri kwenda Dar es Salaam kupokea mwili wa marehemu mume wake wakati
watoto wake wanne wakitangulia Kijiji cha Mtitu Wilaya Kilolo, Iringa
kwa taratibu nyingine za mazishi.
Mama wa marehemu Chaula, Zaina Mpagama, akiwa
kijijini Mtitu, alisema askari huyo ambaye ni mtoto wake wa sita na ni
pekee wa kiume, ameacha pengo lisilozibika... “Baba, nimepata pigo,
mwanangu pekee wa kiume jamani...,” alisema huku akilia kwa uchungu.
Mjini Mbeya, huzuni na simanzi zimetawaka katika
Kambi ya 44KJ Mbalizi baada ya taarifa za kifo cha askari wa miguu,
Peter Werema.CHANZO MWANANCHI
0 comments: