Rasilimali hapa nchini zipo kedekede, isipokuwa mgawanyo wake ndio umekuwa tatizo, huku wazawa wakiamini kuwa wageni wanapendelewa na kujengewa mazingira mazuri zaidi ya kuzifaidi.
Dar es Salaam. Tanzania ni nchi iliyojaliwa rasilimali nyingi na za kila aina.
Ina ardhi kubwa yenye rutuba, misitu , wanyamapori, madini mengi yakiwamo vito vya thamani na hata vyanzo vingi vya maji.
Hata hivyo, miaka 51 tangu ipate uhuru wake na
ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni 45, Tanzania bado ni miongoni mwa
nchi maskini duniani.
Licha ya Serikali kubadilisha mfumo kutoka sera
yake asili ya ujamaa na kujitegemea ambayo iliiwezesha kumiliki
rasilimali zote hadi miaka ya 1980 na kuhamia kwenye mfumo wa soko
huria, bado rasilimali zake hazijawanufaisha Watanzania.
Katika mfumo huria, kumekuwa na sera za uwekezaji
ambazo zimewezesha watu wengi wenye mitaji kutoka nje ya nchi kupewa
rasilimali , kuzitumia kwa uzalishaji.
Tangu mwanzoni mwa mwaka 1990, kumekuwa na
uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta ya madini ambapo kampuni kubwa za
madini duniani zimemilikishwa migodi ya madini, hasa dhahabu.
Hata hivyo, kutokana na kasoro za hapa na pale,
Tanzania bado haijafaidika na madini hayo huku maeneo mengi
yanakochimbwa madini hayo yakikithiri kwa migogoro na umaskini mkubwa.
Kumekuwapo pia na uwekezaji katika sekta ya kilimo
ambapo wawekezaji kutoka nje wamepewa maeneo makubwa ili kuendesha
kilimo cha kisasa cha mashamba makubwa.
Kilimo hiki nacho hakijaifikisha nchi mahali pa kujivunia huku wakulima wengi wakiendelea na kile cha jembe la mkono.
Gesi na mafuta: Wapi tuendako
Hivi karibuni baada ya serikali kupitia Shirika la
Maendeleo ya Petroli (TPDC) imekuwa ikiainisha maeneo inakopatikana
gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
0 comments: