Hadi sasa, Serikali haina habari yoyote ya ukweli kuhusu yaliyofanyika Westgate. Kamera za hivi punde zaonyesha baadhi ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakipora bidhaa kutoka katika maduka na benki ndani ya jengo la Westgate badala ya kuokoa watu.
Matarajio makubwa ya Wakenya yalikuwa kwamba jeshi lao litapambana na magaidi na kuwaokoa wananchi na mali zao, lakini matokeo yakawa kinyume.
Nairobi. Ni zaidi ya mwezi mmoja tangu Kenya ishambuliwe na magaidi wa Al-Shabaab.
Baada ya moshi kutokomea na waliouawa kuzikwa huku
majeruhi wakiendelea kuuguza majeraha yao, maswali mengi bado
hayajapata majibu.
Oktoba 18, runinga moja ya hapa nchini iliweka
bayana kwenye habari zake jinsi mambo yalivyofanyika ndani ya jengo la
Westgate tangu wavamizikuwasilia wakiwa wanaendesha gari ambalo
walilinunua Septemba 6, mwaka kutoka kwa Mkenya mmoja ambaye hakujua
kwamba alikuwa anawauzia watu wenye mpango mbaya.
Mpango ulivyosukwa
Kamera za usalama kwenye Benki ya Barclays iliyoko
kwenye Barabara ya Mama Ngina, jijini Nairobi, zilinasa wavamizi wawili
wakiingia kwenye benki hiyo na kutoa Sh365,000 (Sh6,840,000 za
Tanzania) kutoka katika akaunti zao za kumlipa aliyekuwa amewauzia gari
hilo.
Ndani la gari hilo siku ya tukio kulikuwa na
wavamizi wanne ambao sasa majina yao yamejulikana baada ya uchunguzi wa
kina wa ushirikiano wa Marekani, Israel na Uingereza kuwa ni Abu Baraa
Al Sudani, Khatab Alakene, Umir Al Mogadish na Omar Abdulraham Nabhan.
Wavamizi hao walikuwa wamepanga shambulizi hilo kwa umakini na wakafanikiwa kutekeleza kitendo chao cha kinyama bila kunaswa.
Si ajabu kwamba huenda walisaidiana na adui zetu
kuvamia nchi ya mama yao. Tangu mwaka 2006 Kenya imekuwa ngome ya waasi
ya al-Shabaab na mitandao yao ilikuwa imekita mizizi hasa katika eneo la
Pwani, Kaskazini mwa nchi na Nairobi.
Jijini Nairobi, katika eneo la Eastleigh, asilimia
98 ya wakazi ni wenyeji wenye asili ya Somalia na ni kitovu cha
Al-Shabaab nchini Kenya. Hapa ndipo ramani ya Westgate ilisomwa kwa
makini na wavamizi walipokuwa wakijitayarisha kutekeleza maovu yao.
Inaaminika walipiga kambi kwenye nyumba mbili za wageni katika barabara za Eastleigh.
Uvamizi huo ulifanyika peupe hivyo Polisi na Jeshi
hawawezi kujitetea kwamba hawakuwa wanajua yote yanayopangwa na waasi
wa al-Shabaab.
0 comments: