Unaweza kujiuliza nani anasema kweli katika hili, hakuna shaka jibu litapatikana
Dar es Salaam. Wiki mbili baada
ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya CCM, Chadema,
CUF, NCCR Mageuzi na UDP Ikulu mjini Dar es Salaam na kukubaliana mambo
mawili makubwa kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, vyama visivyo wa uwakilishi bungeni vimeeleza kuwa
havikushirikishwa katika kikao hicho.
Viongozi wa vyama hivyo vidogo waliibua hoja hiyo
katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi uliofanyika Dar es Salaam, kueleza kuwa
Rais Kikwete alitoa kauli ya kutaka vyama vyote viwasilishe maoni,
hakubagua chama chochote cha siasa.
Katika mkutano huo wa ndani, viongozi hao
walimrushia makombora mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
wakidai kuwa yeye na wenyeviti wenzake wametoa maoni ya vyama vyao, siyo
ya vyama vyote 20 vya siasa vilivyopo nchini na kwamba
hawakushirikishwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Peter
Kuga Mziray (PPT Maendeleo) anasema kutokana na hali hiyo vyama hivyo
navyo vimeomba kuonana na Rais Kikwete ili kutoa maoni yake.
Jaji Mutungi kwa upande akalazimika kutumia
busara kupoza mvutano huo, huku akivionya vyama hivyo kujenga utaratibu
wa kushirikishana katika kila jambo.
Katika mkutano wa Bunge uliopita wabunge wa
Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wa muswada huo bungeni
wakipinga matayarisho yake kutoshirikisha upande wa Zanzibar na pia
walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya muswada huo.
Baada ya muswada huo kupitishwa, vyama hivyo
viliungana na kutangaza kufanya maandamano makubwa, Oktoba 10 mwaka huu,
ambayo hata hivyo hayakufanyika baada ya Rais Kikwete kuwaita Ikulu
wenyeviti wa vyama hivyo na hatimaye kukubaliana.
Rais Kikwete na viongozi wa vyama hivyo
walikubaliana kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni
na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili
ifafutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya
sheria hiyo.
Pia, walikubaliana kuwa vyama vya siasa nchini
viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na
maridhiano ili kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi
huku, huku Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kikipewa jukumu la
kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.
Hali ilivyokuwa
Akitoa ufafanuzi wa jinsi vyama visivyo wa
uwakilishi bungeni vilivyotoswa kutoa maoni yao, Mziray anasema: “Vyama
vyetu ndani ya TCD vinawakilishwa na mwenyekiti wa UPDP, Fahm Dovutwa.
0 comments: