NA SISIS TUSHIRISHIKISHWE BUNGENI KATIKA KATIBA MPYA ''BUTIKU''


Dar es Salaam/Mikoani. Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku amesema ipo haja kwa tume iwezeshwe kushiriki mchakato wa Katiba katika hatua zote zilizosalia, badala ya kubaki nje ya Bunge la Katiba kama washauri baada ya kukabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba kwa Rais.
Butiku alisema licha ya umuhimu huo, tume haiwezi kulazimisha kushiriki kwake katika hatua za utunzi wa katiba zilizobaki na kwamba suala hilo linabaki mikononi mwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwapo litaifanyia marekebisho sheria husik                                              Butiku ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere alikuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, kuhusu mchakato wa uandikwaji wa Katiba Mpya, ambao umezua mivutano ya kimasilahi miongoni mwa makundi ya kisiasa.
Moja ya vipengele vya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa na Bunge Septemba, mwaka huu, kinaeleza kuwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba kwa Rais, wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hawatahusika tena na mchakato huo, badala yake watabaki kuwa washauri tu.

“Sisi (Tume) tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria, sheria kwanza ilisema tutafanya kazi mpaka mwisho, sheria ya sasa inasema tutaishia nje ya Bunge kama washauri. Sasa hayo ni mambo ya Bunge, lenyewe liamue wanayoyaamua, wakituhitaji kwenda (bungeni) kwa ushauri tutakwenda. Nadhani itakuwa vizuri hivyo, maana kazi hiyo siyo ya mmoja na inahitaji umakini mkubwa,” alisema Butiku na kusisitiza:

“Kama Bunge litaona inafaa hivyo, ndiyo kazi yetu hatuna kipingamizi, tutakwenda.”

Alitoa kauli hiyo baada ya kuhojiwa kuhusu kuwapo taarifa zilizodai kwamba wajumbe wote wa tume wamepanga kujiuzulu iwapo sheria iliyopitishwa na Bunge haitarekebishwa, ili kuwapa nafasi ya kisheria ya kufanyia kazi Rasimu ya Pili ya Katiba hatika hatua zote badala ya kubaki kuwa washauri.

“Na labda niseme tu kwamba tishio la wajumbe wa tume kutaka kujiuzulu halipo, tishio hilo halipo,” alisisitiza Butiku ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.
Aliongeza kuwa kilichoikasirisha tume ni mwelekeo wa makundi mbalimbali hasa ya kisiasa kuingilia mchakato wa Katiba, hali iliyoifanya tume kuamini kuwa vyama vilikuwa vimeanza kuvuruga mchakato huo.

Hata hivyo, alisema hivi sasa inaonekana kama kila mmoja amerejea kuheshimu sheria na kila mmoja anatimiza wajibu wake.

Mvutano wa kisiasa

Akizungumzia mvutano ulioibuka kati ya vyama vya upinzani na Serikali kuhusu baadhi ya marekebisho yaliyofanywa kwenye sheria, Butiku alisema: “Mimi sitaki kusema kama huo ni mvutano, hiyo ni tofauti ya mawazo. Tusishangae, hamuwezi kufanya jambo kubwa namna hii la kujenga misingi ya taifa letu, kutazama Katiba yetu iweje, mwendesheje nchi yenu bila kutofautiana kimawazo.”
Share on Google Plus

0 comments: