LAMPEDUSA ; KIVUTIO HATARI KWA WAHAMIAJI HARAMU...

  • Kisiwa cha Lampedusa hapo awali kilikuwa na wakazi 5,000, lakini katika miaka ya karibuni, pamekuwa pahala maarufu ambako Waafrika wanakimbilia. Mwaka huu pekee wameshawasili zaidi ya 30,000, lakini maelfu wengine wamezama baharini wakiwa katika safari hiyo ya hatari.  Wakimbizi hao wanaamini kwamba wakitia mguu Lampedusa ina maana wameshaukata, kama wanavosema vijana wa siku hizi au “wameshafika mtoni”.


Vijana wengi hutamani kwenda majuu bila kujua kwamba maisha ya huko si ya kutamani kama huna kazi ya kufanya.Matokeo yake wengi hupata matatizo na wengine kutoswa baharini.
Lampedusa ni kisiwa kidogo cha Italia katika Bahari ya Mediterranean, kikiwa na eneo la kilomita 21 za mraba na wakazi 5,000, hakiko mbali sana na mwambao wa Afrika Kaskazini.
Katika miaka ya karibuni, Lampedusa pamekuwa pahala maarufu ambako Waafrika wanakimbilia. Mwaka huu pekee wameshawasili zaidi ya watu 30,000, lakini maelfu wengine wamezama baharini wakiwa katika safari hiyo ya hatari.
Wakimbizi hao wanaamini kwamba wakitia mguu Lampedusa ina maana wameshaukata, kama wanavosema vijana wa siku hizi au “wameshafika mtoni” – Ulaya, wanayoifikiria kuwa ni peponi.
Mwanzoni mwa mwezi huu zaidi ya wakimbizi 300 walizama ndani ya boti iliyosheheni zaidi ya abiria 500 wakitoka Misrata, Libya.
Siku kumi baadaye wengine 26 walizama katika boti nyingine karibu na Kisiwa cha Malta wakitaka pia kufika Ulaya. Ni maafa ya kusikitisha na katika nchi za Umoja wa Ulaya kuna watu wengi wanaotaka iweko siasa mpya kuelekea wakimbizi, siasa ya kiutu.
Kiini cha tatizo
Lampedusa, kwa sura nyingine ni alama ya mizozo ambayo kiini chake ni serikali zinazotawala vibaya na kutowajali raia katika nchi kadhaa za Afrika
Wengi wa wakimbizi wa Kiafrika wanaovuka Bahari ya Mediterrenean na kwenda Italia wanatoka Somalia, Eritrea na Ethiopia. Utawala wa kidikteta wa Eritrea unawatisha na hauwapi nafasi raia kupumua.
Huko Somalia zaidi ya miaka 20 hakujakuweko na serikali ya maana. Wakimbizi wa kutoka nchi nyingine za Afrika wanatafuta hifadhi Ulaya wakichoshwa na hali duni ya kuwa na mustakbali bora wa maisha. Wanahisi ni bora wajichovye na waelekee hata kusikojulikana, licha ya hatari nyingi zilioko mbele yao.
Utaona familia nyingi za Kiafrika huchanga fedha angalau mmoja wa vijana wao ajitose na asafiri hadi Ulaya kama mkimbizi na huko akatafute maisha. Matarajio ni kwamba pindi kijana huyo atafanikiwa basi huenda atapeleka nyumbani fedha na kuwafaidisha jamaa zake.
Hata hivyo, kwa vijana wengi mambo hayaendi kama walivyoyatazamia. Fedha walizochangiwa humalizikia katika mikono ya walanguzi makatili ambao ni mawakala wa safari hizo za magendo.
Share on Google Plus

0 comments: