KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu na muziki Baby Joseph
Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa nguo zake za ndani
alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni jijini Dar.
Chanzo cha habari ambacho ni shosti wa karibu wa mwanadada huyo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitiririka:
“Alizifua
kama dazeni nzima hivi na kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake.
Heh! Kumbe vibaka hawaachi kitu, waliruka fensi wakazichukua pamoja na
ndala.”
Katika kujua ukweli wa habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta
Baby Madaha na alipopatikana alisema ni kweli alilizwa nguo hizo na
kudai anafanya jitihada za kuhama kwani eneo analoishi limezidi kwa
wizi.
0 comments: