Chama cha
Demokrasia na Maendeleo, Chadema kimeibuka jana bungeni na kusema Serikali
inafahamu ukweli wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa chama hicho
jijini Arusha.Chama
hicho kimesema Serikali ilitumia kutokuwepo kwao bungeni kupotosha wananchi
kuhusu hali halisi juu ya mlipuko wa bomu hilo uliotokea wakati chama hicho
kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Viwanja vya
Soweto jijini Arusha, Juni 15, mwaka huu. kabla ya kuanza kuchangia muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2013/2014, Waziri
kivuli wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa Chadema, Halima Mdee alisema,
“Kabla sijaanza kuchangia Mheshimiwa Spika naomba nianze kwa kuwapa pole wakazi
wote wa Arusha kutokana na mlipuko wa bomu uliosababisha watu kupoteza maisha,
kwani tangu limetokea tukio hilo leo ndiyo nazungumza kwa mara ya
kwanza,”
“Tunazilaani
kauli potofu zilizotolewa na Serikali hapa bungeni, Serikali inajua nini
kilichotokea Arusha na ilitumia kutokuwepo kwetu kupotosha,”
alisema.
0 comments: