HAUSIGELI mmoja nchini Kenya amenaswa akimnyonyesha mtoto wa bosi
wake. Hausigeli huyo aitwaye Grace Mwikali Mwema amekutwa akifanya
kitendo hicho siku mbili tangu aanze kazi japo jaribio lake
halikufanikiwa kwa kuwa mtoto alikataa kunyonya.
Mama wa mtoto aligundua tukio hilo kutokana na kamera aliyoitega nyumbani kwake na akuunganisha na simu yake ya mkononi.
Msichana huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi akisubiri kupandishwa kizimbani.
0 comments: