Na Richard Bukos
KIPA Juma Kaseja kwa mara ya kwanza jana alifika katika Mahakama ya Kazi jijini Dar kusikiliza kesi inayomkabili ya kuvunja mkataba wake na Yanga.Kaseja alifika mahakamani hapo akiambatana na Wakili Nestor Mwenda kutoka Mbamba Advocate lakini hakuzungumza chochote.
Kesi hiyo ilishindikana kuendelea kusomwa kutokana na ofisi ya mawakili ya Mbamba Advocate ambao ndiyo wanaomsimamia Kaseja kudai kuwa iliungua na moto, hivyo nyaraka nyingi zikapotea.
Taarifa kutoka mahakamani hapo zimeeleza kuwa upande wa utetezi wa Kaseja uliomba upatiwe nyaraka nyingine za madai yao kutoka Yanga kwa kuwa zote walizokuwa nazo ziliungua na moto.
Upande wa walalamikaji (Yanga) uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Frank Chacha.
Kutokana na tukio hilo la moto, kesi hiyo iliahirishwa mpaka Machi 10, mwaka huu ambapo itatajwa tena mahakamani hapo baada ya Yanga kupeleka nyaraka nyingine kwa Kaseja.
JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778

0 comments: