Bao la Cannavaro bado lamvuruga katibu Simba

Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Na John Joseph
INASHANGAZA na kusikitisha, lile bao la beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mechi dhidi ya Coastal Union, wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, limeendelea kumvuruga Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally.
Ikumbukwe baada ya Cannavaro kufunga bao hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic aliyekuwa uwanjani, alisimama huku Cannavaro akienda kushangilia kwa kumkumbatia askari wa kike uwanjani hapo, kisha gazeti hili kuripoti stori hiyo, lakini Steven Ally alikuja juu na kulaumu juu ya kuandikwa kwa habari hiyo ya kocha wao kusimama.
Katibu huyo amekuwa akilalamika kila anapopigiwa simu na waandishi wa gazeti hili na kutoa shutuma kuwa linamchafua kocha wao.
“Sitaki kuongea na Championi kwani mlimdhalilisha sana kocha wetu katika stori yenu kuwa alishangilia bao la Cannavaro kisha akamkumbatia askari jambo ambalo siyo kweli, hivyo sitaki kuzungumza na mwandishi yeyote  wa gazeti lenu,” alisema Ally.
Hata hivyo, kila alipokuwa akielekezwa kuwa habari hiyo haikusema kocha huyo alishangilia bali alisimama na kukuna kichwa, pia aliyemkumbatia askari ni Cannavaro na siyo kocha, bado katibu huyo alijifanya kichwa ngumu na kukataa kukubali ukweli.
JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778

Share on Google Plus

0 comments: