
Mjumbe wa Bunge la Katiba Kangi Lugola, ametaja msimamo wake wa kuunga mkono serikali tatu kwamba ni kukwepa unafiki.
Lugola, ambaye alisema kwenye kikao cha Bunge la 
Katiba kuwa atakuwa wa mwisho kuisaliti Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya 
Katiba, alisema kinachowasumbua wanasiasa wengi ni suala la unafiki 
ambalo ameapa hatakuwa tayari kulisujudia.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu msimamo wake 
unaopingana na chama chake cha CCM, alisema wanaounga mkono miongozo ya 
vyama kwenye Bunge la Katiba, wanafanya hivyo kwa unafiki na hofu ya 
kisiasa.
 Alisema kitendo cha kupinga Rasimu ya Pili ya 
Katiba ambayo iliwasilishwa na  mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba,
 ni sawa na kupinga mawazo ya wananchi.
“Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya Tume ya Jaji 
Warioba kukusanya maoni ya wananchi na alichokileta bungeni ni matakwa 
ya Watanzania. Leo hii tunaanza kuchakachua kile ambacho alikifanyia 
kazi kwa uaminifu mkubwa?” alihoji Lugola.
Alisema hawezi kukubaliana na dhambi ya unafiki. “Nawataka wana-CCM wenzangu muweze kupima mambo badala ya kuburutwa,” alisema.
Kuhusu muundo wa Muungano, alisema hata sasa hakuna Muungano kwani Zanzibar imeshajitangazia mamlaka yake.
“Kama wanataka kurudisha Muungano, Serikali ya 
Zanzibar inatakiwa ivunjwe ili ieleweke kuwa hakuna Tanganyika na hakuna
 Zanzibar. Sasa hakuna lolote ambalo linaweza kunishawishi kuwa kuna 
Muungano,” alisema Lugola.
“Muundo wa be huyo alisema kuwa serikali tatu 
unawezekana na tayari upo unafanya kazi, lakini ukiwa katika kivuli cha 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema ambaye wiki iliyopita 
aliwatahadharisha wajumbe wenzake dhidi ya hatari kwa wengi kuwaburuza 
wachache.
0 comments: