DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Efatha Ministry.
(Darasa linaendelea lilipoishia....)
"Kuna vitu ambavyo umebeba na vikijulikana ndipo utakapotokea UPONYAJI wako.
Joshua 7:10 “Bwana akamwambia Yoshua, haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?....
MUNGU Alitoa tamko juu ya mji wa Yeriko kwamba ule mji umetolewa kama sadaka kwa BWANA hivyo wasichukue kitu chochote ila dhahabu watazopata watoe kwa BWANA, lakini vingine waue kila kitu. Akani akaviona vya kutamanika akavibeba akaenda navyo. WANAWAKE wengi WANA mapepo kwa sababu wana roho ya kutamani kila kitu; wakiona heleni wananing’iniza kwenye masikio, wakiona kingine kizuri wanachukua! Sio kila kizuri kinakufaa wewe, wacha vingine viwe vya wengine; hili husababisha kinamama wengi kuwa na mateso ya kila aina.
Cha kushangaza baada ya Akani kuleta vile vitu nyumbani ilileta hatari kubwa sana. Wana wa Israel walipoenda kupigana vitani wakapigwa vizuri sana; adui zao waliokuwa wachache kabisa wakawakimbiza wao ambao walikuwa wengi zaidi.
Joshua akamlilia BWANA, BWANA akamwambia, “Umeleta unajisi katika kambi hii”, ndipo wakamkamata Akani wakamuua. Inawezekana hata wewe kuna kitu Fulani katika kambi yako kilicho najisi; inawezekana umekileta wewe, mume wako, watoto wako, wazazi wako, marafiki zako, n.k. Ni vizuri ukifuatilie ni kipi?"
(Usikose Darasa hili, ni wakati wako huu Mwana wa MUNGU wa USHINDI)
CHANZO EFATHA MINISTRY

Mungu akubariki
ReplyDelete