KESI YA ZITTO KABWE DHIDI YA CHADEMA YAPIGWA KALENDA, SASA KUSIKILIZWA TENA MAY 29



Kesi ya maadai iliyofunguliwa na aliyekuwa Naibu Katibu wa Mkuu wa Chama cha Chadema Zitto Kabwe zidi ya chama hicho imeahirisha nakusikilizwa tena hadi mai 29 katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam
Msajiri wa mahakama kuu Amir Msumi aliaihirisha kesi hiyo baada ya Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo John Utamwa kuugua wakati kesi ilipotakiwa kusikilizwa.Katika kesi hiyo Zitto anaomba mahakama itoe zuio kwa kamati au chama chochote kujadili uanachama wake hadi atakapokata rufaa kupinga uamuzi uliomvua uongozi wake katika kikao kilichofanyika nov 22 mwaka jana ili akate rufaa katika Baraza kuu la chama.
Aidha anaomba chadema isiingilie kazi zake za bunge au uwanachama wake.Zitto alifungua kesi hiyo dhidi ya Baraza la wazamini wa chama hicho pamoja na Dr Slaa.Kabla ya kesi hiyo haijisikilizwa mahakama ilitoa amri kwa kamati kuu au chombo chochote cha chadema kutokujadili uwanachama wa Zitto hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Share on Google Plus

0 comments: