TWASIRA ZA KIKAO CHA KISOMWA KWA RIPOTI ZA CAG ZILIZOPELEKEA MEYA WA BUKOBA KUJIUZULU

Kutoka kushoto: Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh wakiingia ukumbini leo mjini Bukoba.
Viongozi hao wakifungua kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum ya CAG.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila akifungua kikao.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akimkaribisha mgeni rasmi leo kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum " Exit Meeting" cha CAG.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh akisoma ripoti ya ukaguzi maalum leo Bukoba.
Baadhi ya waliohudhuria kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Bukoba katika kikao hicho. Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kushoto) wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bw. Fabian Massawe (kati) katika meza kuu.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (katikati) akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick Utouh. Viongozi meza kuu wote walikuwa makini  kusikiliza taarifa hiyo ya Ukaguzi. Taswira ya kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.Madiwani wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mstahiki Meya Anatory Amani ambaye madiwani wa manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
 **
MEYA wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani amejiuzulu wakati Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Khamis Kaputa na wakuu wa idara tatu ambao ni Mhandisi Nimzihilwa, Ofisa Ugavi Baraka Marwa na Mweka Hazina Ulomi wakivuliwa uongozi baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh iliyosomwa leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera kutatua mgogoro uliokuwepo katika manispaa hiyo.
Share on Google Plus

0 comments: