MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AWATAKA WANA ARUSHA KUACHA USHABIKI WA KISIASA UNAOHATARISHA AMANI

 
Msajili  wa vyama vya siasa  nchini  Bw Fransis  Mutungi  amewataka  wananchi  wa  Mkoa  wa  Arusha na watanzania  kwa  ujumla   kuepuka kuingiza  ushabiki  kwenye  siasa  kwani   kufanya  hivyo  licha ya kuwa  chanzo   cha kuhatarisha  amani  wanaharibu   lengo  la  fani hiyo  ambayo ina  umuhimu  na  faida  kubwa  katika  jamii   kama  taratibu  na misingi yake  ikifuatwa   na kuheshimiwa .
Akizungumza  na wananchi na viongozi wa  ngazi mbalimbali  za  Mkoa  wa  Arusha  waliokusanyika  katika  uwanja  wa  Shekh Amri  Abeid  kuuombea mkoa  wa Arusha amani  Bw  Mutungi  amesema amani ndio msingi  wa  kila  kitu  na  haihusiani kabisa  na  siasa hivyo  hakuna sababu ya  watanzania  kukubali  amani  iliyopo ivurugwe  na  watu  wachache  wanaosingizia  siasa  kwani  wanaopenda amani  ni  wengi  kuliko  wanasiasa 
 
Wakizungumza  katika  hafla hiyo   viongozi wa ngazi mbalimbali  akiwemo   shekh mkuu  wa  mkoa   shabani  bin jumaa  na  askofu  mkuu  wa  kanisa  la  evengelisim centre   eliud  wamewaomba  viongozi  wa  kisiasa  na  wanaotarajia  kutafuta  nafasi za  uongozi   kuwajengea  wananchi  utamaduni  wa  kuheshimi  sheria    na  dola  iliyoko madarakani  kwani    wakizoea  kuvunja  sheria   watafanya hivyo  hata  uongozi  ulioko  madarakani ukibadilika .
 
Mkuu wa  mkoa  wa   arusha  Bw  Magesa  Mulongo  amesema  upo uwezekano  wa  kuendesha  siasa, kudai  haki    na  hata  kukosoa na kutoa  mapendekezo   bila  kuvuruga amani.
 
Wananchi hao  wakiwa  na viongozi wa  ngazi mbalimbali  wakiwemo  wa  kisiasa ,viongozi wa dini  na  wa  mila  walikusanyika katika uwanja   huo  kuhubiri na  kuuombea  mkoa  wa  arusha  amani  unaoandamwa  na  heka heka za  kisiasa  ambazo zimesababisha  kuyumba kwa  uchumi.

-ITV
Share on Google Plus

0 comments: