WE WISH YOU A WONDERFUL, LOVELY $ HAPPY NEW YEAR 2014...STAY CALM
KILI STARS YAIVUA UBINGWA UGANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI - KUKIPIGA NA HARAMBEE DEC 10
Mchezo huo wa robo wa fainali uliochezwa jioni ya leo Kili Stars imefanikiwa kuivua ubingwa The Cranes na kuingia robo nusu fainali baada ya kushinda mikwaju ya penati 3-2 huku kipa Ivo Mapunda akiibuka kuwa shujaa.
Katika dakika 90 timu
hizo zilitoka sare ya bao 2-2, Stars walianza kuongoza kwa mabao mawili
yaliyofungwa na Mrisho Ngassa, lakini Uganda wakasawazisha kupitia
Sserunkuma Dakika ya 16 na Martin Mpuga kipind cha pili katika dakika
73.
Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AWATAKA WANA ARUSHA KUACHA USHABIKI WA KISIASA UNAOHATARISHA AMANI
Msajili wa vyama vya siasa nchini Bw Fransis Mutungi amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuepuka kuingiza ushabiki kwenye siasa kwani kufanya hivyo licha ya kuwa chanzo cha kuhatarisha amani wanaharibu lengo la fani hiyo ambayo ina umuhimu na faida kubwa katika jamii kama taratibu na misingi yake ikifuatwa na kuheshimiwa .
Akizungumza
na wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Arusha
waliokusanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid kuuombea mkoa wa
Arusha amani Bw Mutungi amesema amani ndio msingi wa kila kitu
na haihusiani kabisa na siasa hivyo hakuna sababu ya watanzania
kukubali amani iliyopo ivurugwe na watu wachache wanaosingizia
siasa kwani wanaopenda amani ni wengi kuliko wanasiasa
Wakizungumza
katika hafla hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo shekh
mkuu wa mkoa shabani bin jumaa na askofu mkuu wa kanisa la
evengelisim centre eliud wamewaomba viongozi wa kisiasa na
wanaotarajia kutafuta nafasi za uongozi kuwajengea wananchi
utamaduni wa kuheshimi sheria na dola iliyoko madarakani
kwani wakizoea kuvunja sheria watafanya hivyo hata uongozi
ulioko madarakani ukibadilika .
Mkuu
wa mkoa wa arusha Bw Magesa Mulongo amesema upo uwezekano wa
kuendesha siasa, kudai haki na hata kukosoa na kutoa
mapendekezo bila kuvuruga amani.
Wananchi
hao wakiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa kisiasa
,viongozi wa dini na wa mila walikusanyika katika uwanja huo
kuhubiri na kuuombea mkoa wa arusha amani unaoandamwa na heka
heka za kisiasa ambazo zimesababisha kuyumba kwa uchumi.
-ITV
DK SLAA NA MBOWE APOKELEWA KWA MABANGO YA KUJIUZULU MKOANI KIGOMA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amepokewa kwa mabango katika mkutano wake wa hadhara wilayani Kakonko, Kigoma lakini akawaambia waliofanya hivyo kuwa chama chake hakitayumbishwa huku akiwataka wanaosimama na mabango kumtetea Zitto Kabwe kung’oka naye ndani ya chama.
Dk Slaa yuko mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya
ziara yake ya siku 11 kutembelea Mikoa ya Shinyanga na Kigoma kukagua na
kuimarisha uhai wa chama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Mwenge Kakonko, Dk Slaa alisema Chadema ni chama imara
na kinaendeshwa kwa misingi ya katiba na kanuni.
“Hakuna kiongozi aliye juu ya katiba, ninawaasa wote wanaobeba mabango kujiangalia kwa kuwa ninafahamu wanatumiwa.”
Kabla ya kupokewa kwa mabango hayo, Dk Slaa
aliyewasili Kakonko saa 5:11 asubuhi akitokea Wilaya ya Kahama,
Shinyanga alikwenda moja kwa moja katika Kata ya Mhange ambako alifanya
mkutano wa hadhara.
Dk Slaa alikumbana na mabango hayo saa 8:45 mchana msafara wake ulipowasili Kakonko Mjini ukitokea Mhange.
Wakati Dk Slaa akiingia katika uwanja wa mkutano,
ulio jirani na Ofisi za CCM Wilaya ya Kakonko, kuliibuka kundi la vijana
wapatao watano wakiwa na mabango mkononi na kuanza kukimbia kuyafuata
magari matatu ya msafara wa Dk Slaa huku wakionyesha mabango yao. Hatua
hiyo iliwafanya polisi waliokuwapo eneo hilo la mkutano kuwazuia na
kuanza kuwatimua lakini mara baada ya Dk Slaa kuteremka katika gari yake
na kuingia uwanjani hapo, aliomba kipaza sauti na kuwataka askari hao
kuacha kuwatimua wenye mabango. “Naomba msiwaondoe waacheni waje...
waruhusuni kwenye mkutano na mabango yao. Waacheni waje hapa …
msiwazuie, waacheni waonyeshe mabango yao na muwaruhusu tu wapite hapa
mbele, msiwapige tafadhali,” alisema Dk Slaa.
Baada ya kauli hiyo, polisi waliwaruhusu vijana
hao watano ambao walibakiwa na mabango manne, moja likiwa limechanika
walipokuwa wanawazuia.
Mabango hayo yaliyokuwa na maandishi ya aina moja,
yalikuwa na ujumbe uliosomeka: “Tanzania Kigoma Kakonko bila Zitto
Haiwezekani”, ‘Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe mnatakiwa kujiuzuru mara moja” na
jingine lilisomeka; “Hatupo tayari kwa kusikiliza lolote bila ya Zitto”.
Mara baada ya kupanda jukwaani Dk Slaa aliwataka
tena wenye mabango kusogea karibu na jukwaa kuu alipokuwa amesimama na
kuanza kuwauliza maswali vijana hao iwapo wanajua Katiba ya Chadema na
kama wana kadi za chama. “Naomba niwaulize, hivi nyie wenye mabango
mnaijua Katiba ya Chadema?” Walimjibu: “Hapana.” Dk Slaa akawauliza
tena: “Sasa mnadai nini kwa mabango yenu kama hamjui Katiba ya Chadema?”
Mmoja wa walioshika mabango hayo alijibu: “Mtetezi wetu Zitto.”
Kutokana na hali hiyo Dk Slaa aliwauliza, atakuwa
amekosea akiwakabidhi kwa Polisi kuwa siyo wanachama wa Chadema lakini
wanafanya vurugu katika mkutano halali?
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments: