WALIOWAFANYIA VURUGU PRISONS WAPELEKWA JELA

Mbeya. Watu watano kati ya sita waliokuwa wakishtakiwa kwa makosa ya kuwashambilia wachezaji wa timu ya Tanzania Prisons na kuharibu gari lililokuwa limewabeba, juzi walihukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh 300,000 kila mmoja.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi katika Mahakama ya Mwanzo jijini Mbeya baada ya kupatikana na kosa la kuharibu mali ya timu hiyo ikiwamo kuvunja vioo vya gari baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine jijini hapa siku ya Jumanne.
Waliohukumiwa kwenda jela lakini walijiokoa kwa kulipa faini ni Brayson Shaibu, Vicent Ramadhan, Maiko George, Emmanuel Ndalo na Enock Jeremia wakati aliyeshinda kesi hiyo ni David Laurence .
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa mahakama hiyo, Sadik Mbillu alisema kuwa mahakama hiyo iliridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuwakuta na hatia watu watano kwa kosa la kuharibu mali ya Magereza.
Share on Google Plus

0 comments: