HATUA YA MAKUNDI MTIFUANO LIGI YA MABINWA ULAYA

 
Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya 2013/14 itaanza kesho na keshokutwa, ambapo jumla ya timu 16 zitaingia uwanjani kesho na timu nyingine 16 zitaingia uwanjani keshokutwa.
Timu hizo, pia zinatarajiwa kurudiana baada ya wiki mbili, ambapo zitaingia uwanjani Oktoba 1 na 2.
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ni Bayern Munich ambao walitwaa kombe hilo baada ya kuichapa Borussia Dortmund mabao 2-1 katika mechi ya fainali.
Kundi A; katika kundi hili zipo M
anchester United FC, Bayer 04 Leverkusen, Real Sociedad na FC Shakhtar Donetsk.
Hii ni mara ya 18 kwa Manchester United kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa kocha wao David Moyes ni mara ya kwanza, pia hii ni mara ya kwanza kwa kocha wa Leverkusen, Sami Hyypia ambaye alitwaa taji hilo mwaka 2005 akiwa mchezaji wa Liverpool. Hii ni mara ya pili kwa Real Sociedad kushiriki hatua ya makundi wakati ni mara ya tisa kwa FC Shakhtar Donetsk kushiriki hatua hii.
Kundi B; katika kundi hili zipo Galatasaray, Real Madrid CF, FC København na Juventus.
Kocha wa Galatasaray hivi sasa, Fatih Terim aliwahi kuinoa AC Milan , ambapo alipoiacha AC Milan 2001/02 nafasi yake ilichukuliwa na kocha wa sasa wa Real Madrid, Carlo Ancelotti. Kocha msaidizi wa Galatasaray hivi sasa, Umit Davala alicheza katika mechi saba akiwa chini ya Ancelotti katika klabu ya AC Milan.
Msimu uliopita Juventus walipangiwa kucheza Denmark, ambapo msimu huu pia wamepangiwa kuanza na klabu ya FC København ya Denmark.
Kundi C; katika kundi hili zipo SL Benfica, RSC Anderlecht, Olympiacos FC na Paris Saint-Germain.
Mwaka 1983 katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya timu ya Anderlecht iliichapa Benfica 1-0 huko Lisbon na kutwaa kombe. Kocha msaidizi wa Benfica hivi sasa, Minervino Pietra na mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo, Sheu Han wote walicheza mechi hiyo ya fainali.
Share on Google Plus

0 comments: