
Nawashukuru wasomaji walioniuliza maswali mengi kuhusu na makala nilioiandika wiki iliyopita kuhusu Meri ya kivita ya Konigsberg ya wajerumani ambayo hadi sasa ipo eneo la Rufiji.Wale wanaotaka kwenda kuiona waende hadi kijij cha Nyanisati Wilaya ya mkuranga/kibiti mkoani Pwani ndipo utaelekezwa ilipo.Ikumbuke kwamba kabla ya kuanza kwa vita ya kwanza ya dunia, ujerumani ilikuwa ya kwanza ya dunia , Ujerumani ilikuwa ya kuanza kwa vita ya kwanza ya dunia , ujerumani ilikuwa ikitawa la koloni moja kubwa- Deustch OstAfrika ambalo lilikuwa na nchi za Burundi, Tanganyika na rwanda,.Kwa hiyo
Ziwa Tanganyika ikiwa sehemu ya utawala wake.Graf Van Gotsen hivi sasa MV Liemba, iliitwa jina hilo mwaka 1926 baada ya kutolewa majina na Waingereza na kuitumia tena kama meli ya abiria na mizigo. Wakati huo ilikuwa moja ya meli iliyooletwa na wajerumani.Baadaye ilitumika kama meli ya kivita ikifanya ulinzi katika Ziwa Tanganyika hadi mwaka 1916 ilipozamishwa kwenye mdomo wa mto malagarasi ilipofichwa baada ya wahusika kuogopo kuvamiwa na washirika wa Uingereza, Ubelgili na Ufaransa waliokuwa wakimfurusha Mjerumani hapa Afrika Mashariki.Meli nyingine ilikuwa ikiitwa Somalia na nyingine Kronborg meli hiyo kwakweli haikua ya Wajerumani bali waliiteka kutoka kwa waingereza ikwa wakati huo Rubenes na ilikuwa ni yakusafirisha mizigo ya biashara.Wajerumani walipoiteka wakaaita Kronborg wakatengeneza nyaraka za kughushi ionekane ni meli ya kidenmark na wanafunzi wake waliambiwa wazungumze kidenishi.Meli hii ilitumika kupeleka shehena ya mkaa katika meli ya Konigsberg ambayo wakati huo ilikuwa na matatizo ya kiufundi.Hata hivyo meli hiuo ilishtukiwa na waingereza na kufukuzwa mpaka Manza Bay kaskazini mwa Tanga nchini Kenya ambako iliaribiwa vibaya na meli ya kivita ya waingereza iliyokuwa ikiitwa MSHyacinth ingawa badae wajerumani waliirudia tena kuona kama kuna kitu cha kuchukua kilichosalia kwa ajili ya vita ya aridhini.
Imeandikwa na Dennis Magessa
ENDELEA KUFWATILIA STORI NZURI KUTOKA HABARI KAMILI KAMILI
0 comments: