RECHO AWACHANA MASTAA WANAOJISHUSHA UMRI



STAA wa sinema za Kibongo, Rachael Haule ‘Recho’ (25) amefungua kinywa chake na kuwachana wasanii wenye tabia ya kujishusha umri.
Akitema cheche hizo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya kinasa sauti cha Amani, mwigizaji huyo aliyefanya

poa kwenye sinema yake ya Vanesa in Dillema alisema anawashangaa wanaojishusha umri na kuwaona wana upeo mdogo na imekuwa ni kasumba ya mastaa wengi pindi wanapohojiwa kwenye ‘midia’.
“Daaah! Nakereka sana, kwa nini mtu usitaje umri wako wa ukweli. Mastaa wengi Bongo wanapohojiwa wanajishusha miaka sasa sijui kila siku utaendelea kuwa mdogo, huo ni ujinga,” alisema Recho pasipo kuwataja majina mastaa wenye ‘kamchezo’ hako.
Share on Google Plus

0 comments: