
FAMILIA ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, marehemu Daudi Balali imeingia katika mgogoro baada ya baadhi ya ndugu kudaiwa kugombania mashamba aliyoyaacha marehemu huyo, Amani linakupa ‘ei tu zedi’.
i Marekani, Mei 16, 2008.
Kwa mujibu wa chanzo, ndugu hao wanadaiwa kugombania mashamba hayo yaliyopo Bunju kwa Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Deodatha Elius, ndugu wa marehemu, anadai shamba lake lenye ukubwa wa ekari sita limeuzwa bila yeye kuwa na taarifa.
Alisema eneo hilo alinunuliwa na Balali lakini bahati mbaya hakuwa na hati. Alidai kwamba yeye na Balali ni mtu na binamu yake.
Akizungumza na waandishi wetu juzikati huko Bunju, mwanamke huyo ambaye ni mjane, alisema kuwa kabla ya kuolewa alikulia mikononi mwa marehemu Balali, baada ya kupata mume aliondoka kwenda kuanza maisha mapya.
Alidai baada ya kufiwa na mume mwaka 1997, Balali alimwambia atafute eneo ili amnunulie aweze kuishi na watoto wake watatu aliowapata na marehemu mume wake.
“Nilianza kutafuta eneo, nikapata Bunju kwa Jeshi, kaka Balali akaninunulia eneo hilo kipande kidogo na palikuwa na kibanda cha kuishi. Baadaye kidogo nikapata eneo jingine jirani likiwa na nyumba nzuri, kaka akaninunulia nikawa na ekari sita,” alisema mwanamke huyo.
Alisema alishangaa baada ya kifo cha Balali ndugu zake walichukua jukumu la kuuza shamba lake hilo lenye nyumba bila kumwambia na wanunuzi kumtaka aondoke.
“Kabla Balali hajafariki dunia, hizi fujo hazikuwepo na waliouza eneo hilo ninawajua ni ndugu zetu wa karibu, wamefanya hivyo kwa lengo la kunikomoa,” alisema.
Pia aliziomba taasisi za haki za binadamu kumsaidia ili aweze kuishi na watoto wake kwa raha.
Aliongeza kusema kuwa wakati wa uhai wake, marehemu alihakikisha kila mtu anamsaidia na hata hao ndugu waliouza eneo hilo walipewa maeneo yao.
Baadhi ya majirani wanaofahamu sakata hilo walidai wanaomchezea mchezo mchafu ni ndugu zake wa karibu, kitendo ambacho walisema kinasikitisha.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, mkazi mmoja wa eneo hilo alidai kuwa, marehemu Balali aliwahi kuwaita na kuwaambia kuwa eneo hilo amemnunulia dada yake huyo.
“Ukweli ni kwamba baadhi ya ndugu waache tamaa za mali, wamuache mjane alee watoto wake kama alivyoachiwa eneo hili na kaka yake,” alisema jirani huyo.
Naye mjumbe mstaafu wa Shina Namba 41, Bunju ‘A’ Kilungule, Said Salum ambaye kwa wakati huo alikuwa anajua mipaka ya wenyeji alisema eneo hilo lilikuwa linakaliwa na watu watatu tofauti, hao wote walimuuzia Balali naye akamkabidhi mwanamke huyo kwa kuwaambia asitokee mtu wa kumnyang’anya.
“Kuanzia hapo mama huyo alianza kuishi hapa na kufanyia usafi eneo ambalo lina ukubwa wa ekari sita, sasa tunashangaa kuona mama huyu akipata usumbufu,” alisema mjumbe huyo.
Amani lilifanikiwa kumpata mtu aliyekuwa msimamizi wa mali za Balali kwa wakati huo hadi sasa aliyejitambulisha kwa jina la Bernard Balinzako ambapo alisema:
“Mimi nilikuwa msimamizi wa shughuli za Balali, kweli Deodatha ni mmoja ya ndugu wa marehemu. Ninachokifahamu mimi ni kuwa eneo lilinunuliwa na Balali kama alimkabidhi huyo dada sijui.”
Alisema muuzaji wa eneo hilo ni msimamizi wa mirathi ya marehemu huyo ambaye hakumtaja jina lakini alisema ni dada wa Balali.
0 comments: