WAFAHAMU WANASOKA WENYE FEDHA NYINGI KULIKO WOTE NCHINI KENYA

Usajili wa kiungo wa kimtaifa wa Kenya ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa Harambee Stars Victor Mugubi Wanyama kwenda klabu ya Southampton toka klabu ya Glasgow Celtic umefanya orodha ya wachezaji wenye fedha nyingi kuliko wote nchini Kenya kubadilika .
Mcdonald+Mariga+Maximiliano+Maxi+Lopez+Catania+w0WJanAy1lsx
Nafasi ya tatu inashikiliwa na kaka mkubwa wa Victor Wanyama ambaye ni McDonald Mariga . Mariga aliweka historia ya kuwa mchezaji wa Kwanza toka Kenya na Afrika Mashariki kuvaa medali ya ubingwa wa Ligi ya mabingwa na pia alikuwa mchezaji wa kwanza wa ukanda huu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa . Katika mishahara ya kawaida Mariga anashika nafasi ya tatu lakini anaweza kuwa mchezaji mwenye utajiri kuliko wote kwa kuwa amewekeza kwenye biashara nyingi nje ya soka ambazo zinamfanya awe mchezaji tajiri kuliko wote kwenye ukanda huu. Kimshahara Mariga analipwa milioni 77 za Kenya  kwa Mwaka na hiyo inamfanya kuwa mchezaji wa tatu anayelipwa hela nyingi .
International Friendly: South Africa v Kenya
Nafasi ya pili kwenye orodha hiyo inashikiliwa na nahodha wa zamani wa timu ya taifa Dennis Oliech ambaye amecheza kwenye ligi ya Ufaransa kabla kina Mariga na Wanyama hawajatoka nchini Kenya . Mshahara wa Oliech kwa mwaka ni shilingi milioni 91 za Kenya ambazo kibongbongo ni sawa na shilingi bilioni 1,693,305,779.42 9bilioni moja  na milioni mia sita tisini na tatu , laki tatu na mia saba sabini na tisa na senti arobaini na mbili) . Kwa sasa Oliech anachezea Ac Ajaccio  ya huko huko Ufaransa .
Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Wanyama ambaye kwa sasa pia ni mchezaji ghali kuliko wote waliowahi kuuzwa wanaotoka nchini Scotland . Wanyama analipwa mshahara unaokaribia milioni 250 za Kenya kwa mwaka
kwa mujibu wa mkataba wake ambao haujawekwa wazi kuonyesha atakuwa analipwa kiasi gani kwa wiki.
Victor-Wanyama-scores-for-Celtic-against-Dundee-1341816
Share on Google Plus

0 comments: