STAA HUYU WA SOKA AMEKUA MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJIJLIWA NA CARLO ANCELOTTI

Asier Illarramendi
Klabu ya Real Madrid imemsajili mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Vijana ya Hispania Asier Illarramendi toka klabu ya Real Sociedad kwa dau la Euro Milioni 38 ambapo mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka 6 na Real Madrid ambao unamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya Carlo Ancelotti.
Tayari Madrid ilishamsajili nyota wake wa zamani Daniel Carvajal aliyerudishwa toka Bayer Leverkusen  pamoja na kiungo mwingine wa timu ya vijana Isco toka Malaga lakini usajili wa wachezaji hao wawili (Isco na Carvajal) ulikuwa kwenye  mipango kabla ya kuja kwa Ancelotti.
Illarramendi alikuwa akisakwa na klabu za England kama Liverpool, Arsenal na Tottenham Hotspurs lakini Madrid wameshinda vita ya kusajili ambapo anajiunga na wenzie chini ya Ancelotti kabla ya kuanza kwa
kambi ya kabla ya msimu yaani Pre-Season.
Usajili wa Illarramendi ni muendelezo wa sera ya Rais Florentino Perez ambaye amesema kuwa ana mpango  wa kusajili wachezaji wa Hispania zaidi kuliko wachezaji toka nje ya nchi.hi-res-170609659_crop_exact
Share on Google Plus

0 comments: