PAPA FRANCIS AUDHURIA SIKU YA VIJANA DUNIANI NCHINI BRAZIL


Baba mtakatifu Francis amepokewa kwa vifijo na nderemo na maelfu ya waumini wa kanisa katoliki alipowasili nchini Brazil kuhudhuria siku ya vijana duniani, lakini baada ya mapokezi hayo,kulishuhudiwa maandamano
Papa Francis mwenye umri wa miaka 76 alibebwa katika gari lililo wazi na kuzunguka mji mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro katika ziara yake ya wiki moja katika nchi hiyo ambayo idadi ya waumini wa kanisa katoliki inazidi kudidimia na hatua zake za kiuchumi zimekubwa na ghasia kutoka kwa umma katika siku za hivi karibuni.
Kiongozi huyo mzaliwa wa Argentina ambaye ndiye wa kwanza kutokea mataifa ya Amerika kusini kuliongoza kanisa hilo, alilakiwa na waumini wake lakini askari wa usalama walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwatawanya waandamanaji walioanza kurusha mabomu ya petroli baada ya papa kukutana na Rais wa Brazil Dilma Rousef katika ikulu ya gavana wa jimbo hilo.
Papa Francis akiwapungia waumini alipowasili Rio de JaneiroPapa Francis akiwapungia waumini alipowasili Rio de Janeiro
Siku ya vijana duniani yaadhimishwa
Papa Francis yuko nchini Brazil kuhudhuria siku ya vijana duniani,siku ambayo ilianzishwa mwaka 1985 na papa John Paul wa pili.Siku hii inaadhimishwa rasmi hii leo ambapo takriban vijana milioni 1.5 wanatarajiwa kuhudhuria.
Licha ya ulinzi mkali kutokana na ziara hiyo ya papa ambapo wanajeshi 30,000 na mapolisi wanashika doria, watu kadhaa waliweza kufikia gari la papa na hata kumgusa.Papa huyo alisalimiana nao kwa mikono na kuwabusu watoto.
Jeshi lilitangaza Jumapili iliyopita kuwa liligundua bomu wakati wa kikao cha mazoezi katika choo cha kanisa la Our Lady of Aparecida katika jimbo la Sao Paulo ambako kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea hapo kesho.
Baba mtakatifu amepata umaarufu sana katika miezi minne tangu kuchaguliwa kuliongoza kanisa katoliki kutokana na unyenyekevu wake na kuwajali maskini.
Vijana wengi hawana ajira
Alipokuwa kwenye ndege kuelekea Rio,papa alilalama kuwa karibu kizazi kizima cha vijana kiko katika hatari ya kutojua ni kipi kitokanacho na kazi kutokana na mzozo wa kiuchumi ambao umewaacha vijana wengi bila ajira katika nchi nyingi za ulaya na kuwaacha nyuma vijana maskini wa kutoka nchi zinazoendelea.
Baba mtakatifu Francis akiwasli BrazilBaba mtakatifu Francis akiwasili Brazil
Serikali ya Brazil imetumia dola milioni 52 kwa ajili ya ziara hiyo ya papa lakini haonekani kulengwa na waandamanaji wa Brazil wanaoghadhabishwa na maamuzi ya kiuchumi ya serikali yao.
Kanisa katoliki linazidi kupoteza umaarufu wake nchini humo kutokana na kuinukukia kwa makanisa ya kiinjili na kuenea kwa maadili ya kilimwengu.
Zaidi ya asilimia 90 ya wabrazil walijitambulisha kuwa wakatoliki miaka ya 70 lakini kura ya maoni iliyotolewa Jumapili iliyopita inaonyesha ni asilimia 57 tu ya wabrazil wanaojiita wakatoliki huku asilimia 28 wakisema ni wapentekosti au waumini wa makanisa ya kiinjili.
Papa Francis anatarajiwa kutembelea mitaa duni mjini Rio na kukutana na wafungwa wa umri mdogo katika hatua ya kuendeleza msingi wake wa wito wa kutaka kuona kanisa nyenyekevu linalojitolea kuwasaidia wasiobahatika katika jamii.
Share on Google Plus

0 comments: