Mgomo wa saa 24 wa wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Ugiriki
umeipoozesha kabisa nchi hiyo, huku bunge likitarajiwa hivi leo
kupitisha mpango unaopingwa na wafanyakazi hao wa kukata nafasi za ajira
kwenye serikalini.
Maelfu ya wafanyakazi wenye hasira waliacha ofisi zao na kuandamana
mbele ya bunge la Ugiriki hapo jana, dhidi ya mpango wa serikali
kuwapunguza wafanyakazi wa sekta ya umma, ili kukidhi matakwa ya
wakopeshaji wa kigeni.Mgomo huo dhidi ya mpango mpya wa kuwahamisha au kuwafukuza kaz
i wafanyakazi wa serikali ulifanyika siku moja tu kabla ya bunge kuupigia kura mkururo wa mageuzi ambao lazima upitishwe kabla ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa hawaidhinisha msaada zaidi wa kifedha.
Maandamano makubwa kabisa kuwahi kutokea
Mgomo mkubwa nchini Ugiriki wa tarehe 16 Julai 2013.
Zaidi ya waandamanaji 30,000, wakiwemo polisi wa baraza la
manispaa na walimu ambao wamelengwa kwenye mpango huo wa kuwafuta au
kuwahamisha kikazi, walikusanyika kwenye uwanja wa bunge wakipiga ngoma
na kuweka zogo, katika kile kinachotajwa kuwa moja ya maandamano makubwa
ya kupinga hatua za kubana matumizi kuwahi kufanyika nchini Ugiriki
mwaka huu.Mmoja wa waandamanaji hao, Eleni Fotopoulou, mwenye umri wa miaka 58, aliliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA, kwamba inaonekana kama Ugiriki imeshakuwa maiti na sasa tai wanapigania mzoga wake. Mwanamke huyo ambaye ni mwalimu mstaafu na mama wa watoto wawili, aliongeza "Sina tena hasira, nina fadhaa. Lazima tupambane."
Ugiriki imegawanyika juu ya ikiwa wafanyakazi wa sekta ya umma, ambao kawaida kazi zao zinalindwa na katiba, wanapaswa pia kuyapata maumivu ya kufukuzwa au kuhamishwa kazi, ambayo tayari yamewanamia wale wa sekta binafsi.
Schäuble kupokewa kwa maandamano
Mgomo mkubwa nchini Ugiriki wa tarehe 16 Julai 2013.
Hata hivyo, kimsingi, wote wanakubaliana kwamba jamii ya
Ugiriki haiwezi tena kubeba mzigo wa makato zaidi ya matumizi na
kupandishiwa kodi. Huo ndio ujumbe ambao serikali ya Ugiriki inasema
itampa Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble, anayewasili
mjini Athens hapo kesho.Kuna uwezekano mkubwa, waandamanaji wakajitokeza tena hapo kesho, kumuonesha Schäuble upinzani wao dhidi ya mpango unaopigiwa chapuo na Ujerumani. Wagiriki wengi wanailaumu Ujerumani kwa mgogoro wao wa kiuchumi na picha zinazomuonesha Kansela Angela Merkel kwenye taswira ya mtawala wa Kinazi zimejaa mjini Athens.
Wakopeshaji wa Ugiriki, ambao tayari mara mbili wameshaipa nchi hiyo fedha zifikiazo euro bilioni 240, wamekasirishwa na kiwango kidogo cha maendeleo kilichopigwa, hasa kwenye suala la kuweka sawa sekta yake ya umma yenye wafanyakazi 600,000, ambayo inaonekana kujaa ufisadi na isiyo ufanisi.CHANZO DW
0 comments: