Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kutumia helikopta
yameyashambulia maeneo ya waasi karibu na upande wa mashariki mwa mji wa
Goma, ikiwa siku ya tatu ya mapigano makali yaliyosabaisha wimbi la
ukimbizi.
Katika barua ilitumwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambayo
Shirila la habari la Reuters limepata nakala yake, Kongo imekituhumu
kikosi maalumu chaRwanda kwa kuwasaidia waasi wa M23 katika mapigano hayo. Lakini pia katika taarifa yao walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo wamekanusha madai ya Rwanda kwamba walifyatua makombora dhidi ya nchi hiyo kutoka ardhi ya Kongo Jumatatu.
Taarifa ya jeshi hilo la ulinzi wa amani lijulikalo kama MONUSCO, umesema wanajeshi wake hawajahusika na mapigano katika eneo la Goma na kwa hivyo hawawezi kuhusika katika kufyatua makombora kwenye mipaka ya Rwanda.CHANZO DW
0 comments: