Shirikisho la mchezo wa riadha duniani lasema mfumo wake wa kupambana na
wanariadha wanaotumia madawa ya kuongeza nguvu unafanyakazi, wakimbiaji
mashuhuri Tyson Gay na Asafa Powell wanasa katika mtego,wa Doping.
Shirikisho la mchezo wa riadha ulimwenguni IAAF limesema kuwa kuaminika
kwa mpango wake wa kupambana na wanariadha wanatumia madawa ya kutunisha
misuli kumeimarika na sio kuporomoka baada ya wakimbiaji nyota Asafa
Powell na Tyson Gay wa Marekani kunasa katika mtego huo baada ya
kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu, ambayo
yamepigwa marufuku.Gay , bingwa wa zamani wa dunia ambaye alishinda mbio za mita 100, na 200 katika mashindano ya kitaifa nchini Marekani mwezi uliopita, amesema kuwa atajitoa katika mashindano yajayo ya ubingwa wa dunia nchini Urusi mwezi ujao.
Bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 na 200 duniani Tyson Gay
Wakabiliwa na adhabuPowell ambaye alishikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 hadi Usain Bolt alipoishusha mwaka 2008, pamoja na bingwa wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki Sherone Simpson pia wanakabiliwa ya hatua ya kuzuiwa kushiriki michezo ya riadha baada ya
kupatikana na hatia ya kutumia madawa hayo katika michezo ya chama cha riadha cha Jamaica mwezi uliopita.
Asafa Powell (kulia) akiwa na Nesta Carter
Msemaji wa shirikisho la michezo ya riadha duniani IAAF Nick Davies
amesema shirikisho hilo haliwezi kuzungumzia kuhusu kesi ambazo bado
hazijaamuliwa , lakini ameongeza kuwa mapambano dhidi ya doping
yameimarishwa , na sio kuporomoka , kila mara inapowezekana kufichua
kesi mpya.Wanariadha watano ikiwa ni pamoja na washindi wawili wa medali za olimpiki walipatikana na hatia ya kutumia madawa ya kutunisha misuli katika mashindano ya riadha nchini Jamaica .CHANZO DW
0 comments: