WALIMU KOBORESHEWA MAISHA ILI KUBORESHA MSINGI MZURI WA ELIMU

Kutoka kushoto ni Mtangazaji wa Channel Ten Kipindi cha Mimi na Tanzania Bi Hoyce Temu aliewahi kuwa kushiriki mashindano ya Miss Tanzania akiteta jambo na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha Bwana Amani Gulugwa katika maadhimisho ya miaka 50 tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 1963 ,wawili hao waliwahi kusoma elimu yao ya sekondari katika shule hiyo kongwe, shughuli hiyo iliambatana na uchangishaji wa fedha za ujenzi wa maktaba ya kisasa itakayogharimu kiasi cha shilingi milioni 400.

Mtangazaji wa Channel Ten Kipindi cha Mimi na Tanzania Bi Hoyce Temu aliwahi kuwa kushiriki mashindano ya Miss Tanzania akionyesha cheti cha ushirika katika kufanikisha maadhimisho ya miaka 50 tangu shule ya Arusha Sekondari ianzishwe mnamo mwaka 1963 ,Mtangazaji huyo aliwahi kusoma elimu yake ya sekondari katika shule hiyo kongwe

Wapili kutoka kushoto ni Mbunge wa Arusha Mijini Bwana Godbless Lema akisalimiana na Mwalimu mkuu wa shule ya Arusha Secondary ,Joseph Malamsha mara baada ya kusoma risala yake na kumkabidhi Mgeni rasmi wa kwanza kutoka kushoto ambaye ni Sifaeli Moleli katika maadhimisho ya miaka 50 tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 1963 ,shughuli hiyo iliambatana na uchangishaji wa fedha za ujenzi wa maktaba ya kisasa itakayogharimu kiasi cha shilingi milioni 4000.(picha na Ferdinand Shayo)
shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 2000 ilianzishwa mwaka 1963 huku baadhi ya viongozi na watu maarufu nchini wengi wao wakiwa wamepata elimu yao ya sekondari katika shule hiyo.Akiongea kwa jazba leo mkoani Arusha mbunge wa Arusha mjini Godbless alisema walimu ni lazima waboreshewe msingi mzuri wa maisha yao ili waweze kuwapatia wanafunzi misingi mizuri ya elimu.Moja kati ya wliopata elimu yao ya sekondari ni waziri mkuu mstaafu na mbunge wa munduri Mh Edward Lowasa
Share on Google Plus

0 comments: