ASKARI MAGEREZA WADAIWA KUUA MFUNGWA ARUSHA

Mji wa Arusha kama huonekanavyo kwenye picha
Haruni Sanchawa, Dar na Joseph Shaluwa, Arusha
BAADHI ya wafungwa katika Gereza la Kisongo mjini hapa wamedai kuwa mfungwa Willfred Mallya mwenye namba 315 aliyefungwa mwaka 2003 ameuawa na askari wa magereza baada ya kupewa kipigo kizito  Januari 24, mwaka huu.
Chanzo chetu ndani ya gereza hilo kimedai kuwa, Mallya aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha aliitwa na afande mmoja (jina tunalo) na akapigwa sana kwa amri ya mkubwa mmoja ambaye pia jina lake tunalihifadhi, alipozidiwa aliitwa daktari mmoja ambaye alidai anajifanya kuzidiwa, akamuacha.
Wafungwa hao waliongeza kuwa ilipofika Januari 25, mwaka huu saa 4 usiku Mallya akiwa katika chumba cha adhabu, alifariki dunia na mwili wake ulipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Maunt Meru.
Share on Google Plus

0 comments: