Teknolojia ya video huenda ikafanyiwa majaribio msimu ujao katika ligi kuu za kandanda za baadhi ya nchi baada ya uamuzi wa Bodi ya Shirikisho la Kimataifa la Kandanda – IFAB kuijaribu teknolojia hiyo
Maafisa wa kandanda wa Uholanzi na Uingereza ni miongoni mwa mashirikisho yanayosema kuwa matumizi ya mfumo wa kurudishwa nyuma video na kuangalia tena yanaweza kufanyiwa majaribio katika michuano ya ya ndani.
IFAB inapendekeza kuufanyia majaribio mfumo wa kuwasaidia maafisa wa mechi kupitia video katika sehemu muhimu zinazouathiri mchezo kama vile magoli yenye utata na maamuzi ya penalti. Mipango hiyo itapigiwa kura katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa IFAB mwezi Machi.
Katibu wa IFAB Lukas Brud amesema majaribio hayo yataonyesha namna ya kutumia kwa njia nzuri teknolojia ya video – iwe ni kutumiwa au kutoumiwa video pembeni mwa uwanja au ndani ya gari dogo nje ya uwanja na ikiwa mchuano unapaswa kusitishwa kwa muda au la. Majaribio hayo huenda yakafanywa kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu.
Tenkolojia ya video huenda ikawa hatua ya karibuni kuyafanya maisha ya marefarii wa uwanjani kuwa rahisi, miaka mitatu baada ya IFAB kuidhinisha matumizi ya teknolojia ya kuamua kama mpira umevuka mstari wa lango au la ambayo inatumika katika ligi kubwa na mashindano makuu kama vile Kombe la Dunia.
Teknolojia ya video katika kandanda?
About author: Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: