Mtu mmoja amefariki na wengine watano wako hospitali baada ya majaribio ya dawa nchini Ufaransa kwenda kombo.
Waziri wa afya wa Ufaransa Marisol Touraine amesema leo kuwa watu sita waliojitolea kufanya majaribio hayo walishiriki kula dawa inayotengenezwa na maabara ya ulaya kaskazini magharibi mwa mji wa Rennes.
Kwa mujibu wa vyanzo karibu na mkasa huo, dawa hiyo ni ya kutuliza maumivu yenye Cannabinoids, kiambato kinachopatikana katika mmea wa bangi.
Chanzo kingine kimesema kampuni hiyo inayofanya utafiti ilikuwa inafanya kazi hiyo kwa niaba ya kampuni ya madawa ya Ureno ya Bial.
Waziri wa afya wa Ufaransa amesema ajali mbaya imetokea, na kuongeza kwamba majaribio hayo yamesitishwa na watu wote waliojitokeza kuyafanya wametakiwa kurejea nyumbani.
Mtu mmoja afariki baada ya kutumia dawa za majaribio
About author: Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: