Tanzania yafunga rasmi matangazo ya analojia


Tanzania jana  imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha uzimaji rasmi wa mitambo ya analojia kwa Televisheni huku ikiwa ni miongoni mwa nchi za kwanza za kusini mwa jangwa la Sahara kuingia kwenye mfumo wa digitali.
  
Makamu wa rais wa Tanzania Dakta Mohamed Gharibu Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alizitaka taasisi za masuala ya mawasiliano na utoaji wa habari nchini kusimamia kwa ukamilifu maudhui yanayowafikia wananchi ili yatumike kwa maendelea na kuhakikisha kuwa Chanel za Television hizo hazitoi mafundisho yasiyofaa.
  
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano chini Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kwa kuwa mpaka sasa kuna visimbuzi milioni moja vinavyotumiwa na wananchi kupata matangazo ya televisheni kwa kuzingatia kanuni na sheria..
Share on Google Plus

0 comments: