DC Makonda...sitasahau niligombea chakula cha mbwa...

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
MAISHA usiyapimie! Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema katika harakati zake za maisha, aliwahi kugombea chakula na mbwa wakati akiwa chuoni wilayani Bagamoyo, kitu ambacho kilimuumiza mno.
Makonda alitoa maneno hayo wakati akizungumza katika semina ya kujikomboa kutoka katika umasikini inayofanyika kila Jumapili katika Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Makumbusho jijini Dar es Salaam ambayo mhamasishaji mahiri nchini, Eric Shigongo hushiriki.
“Mama yangu alikopa Finca, hela hazikutosha ada, vitu vyake vyote vya ndani vikachukuliwa, chuoni nilikuwa nasubiri wenzangu wakishakula kantini, nawahi kula makombo kabla watu waliotoa oda ya chakula cha mbwa hawajaja. Wakati mwingine nililazimika kugombana na watu waliokuja kuwachukulia hao mbwa kama tukikutana.
“Siku moja Bi. Mkubwa alikuja shuleni na mzigo wa unga bila mboga, hakuwa na chochote na wala mimi sikuwa na fedha. Nilifanya bidii kwenye masomo hatimaye leo hii mimi ni mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kama mimi nilitokea huko na niko hapa leo, ni wazi kuwa hata nyinyi mnaweza kubadilika na kuwa watu wengine kabisa katika maisha,” alisema Makonda, mmoja wa vijana wengi waliopewa nafasi za juu za uongozi na serikali ya awamu ya nne.
Kwa simulizi zaidi ya Paul Makonda, usikose kufuatilia magazeti ya Global Publishers.
Share on Google Plus

0 comments: