HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Katinbu mkuu wa Tughe Taifa Ally Kiwenge alisema jana kuwa pamoja na hatua hiyo ya kisheria kuchukuliwa dhidi ya mbunge huyo ya kutaja hadharani mshara wa rais kitendo ambacho nikinyume na sheria ya kazi na mahusiano kinachosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa.
''Huu sio wakati wa wakujua mshahara wa rais au wa waziri mkuu ni wakati ambao wabunge wanapaswa kupigania mishahara y awafanya kazi ili iboreshe na kuweza kukidhi mahitaji yao binafsi na si vinginevyo" alisema hayo kiwenge alipokua akitolea maelezo swala hilo lililowahudhii wafanyakazi wa serikali
0 comments: