Miezi kadhaa ikiwa imepita tangu mtayarishaji na mwigizaji wa filamu nchini Jennifer Kyaka ‘Odama’ kuanza kumiliki vifaa vya kisasa kwa ajili ya utengenezaji filamu, amesema kitu kinachomuumiza zaidi ni kwa baadhi ya watayarishaji kuamini kwamba fedha wanazotumia waigizaji wa kike kuandalia filamu wamehongwa.
Akizungumza na gazeti hili, Odama alisema hata maendeleo yake hayajatokana na kuhongwa.
Anaongeza kuwa watayarishaji wa kike wamekuwa na
changamoto nyingi sana katika uandaaji wa filamu nchini, lakini yeye ni
mwanamke wa shoka kwani anajiamini kwa kile anachokifanya.
“Kinachoniumiza ni hawa wenzetu kuamini kuwa
watayarishaji wa kike fedha zao za kupewa na hawana uchungu nazo, hata
wakipatana na wasanii kucheza katika filamu zao gharama huwa kubwa
tofauti na waandaaji wa kiume wanaonekana wahangaikaji,” alisema.
“Ninatengeneza filamu bila kutegemea nguvu ya mtu
yeyote kutoka nje, ndiyo maana nimeweza kufanya kazi zenye ubora ikiwamo
‘Jicho Langu’. Unaweza kujiuliza mambo mengi sana juu ya maneno haya
‘Jicho Langu’. Hii ni filamu iliyoandaliwa chini ya kampuni ya J-Film 4
Life,” alisema Odama.
Alisema ubora wa kazi hiyo unaweza kukuzwa na
Watanzania ambao watanunua kopi halali ili kukuza uchumi wa nchi na
msanii. “Tatizo tunalokumbana nalo hasa ni wapenzi wa filamu kukimbia
kopi halali na badala yake kununua kopi zisizo halali, mwishowe
wanawafaidisha watu wengine.”
Hata hivyo, Odama alisema uamuzi alioufanya kwa
kuamua kukua kisanii umempa matunda makubwa na kumfanya awe imara katika
utayarishaji wa filamu bora wakati wote kwa kutumia kampuni yake ya
J-Film 4 Life ambayo inaleta changamoto kwa kampuni nyingine za filamu.
“Ninapofanya kazi nikiwa nimesimama kama Odama
kunakuwa na utofauti.Unapokuwa chini ya mtu au kuwa tegemezi , ni vigumu
kuwa mwenye ubunifu sana na mwenye mafanikio mazuri.
0 comments: