
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi chini ya ulinzi.
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi
Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.

Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania (EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi
Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe akiwa anatolewa
mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

Watoto
wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of
Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka
Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo

Mtoto
wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of
Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na
waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika

Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
![]() |
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30 |

MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi
Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na
viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba
Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo
amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na
Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema
Beni(19).
Amesema
Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008
hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha
130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002
kwa kosa la ubakaji.
Kutokana
na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta
Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi
uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa
akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya
kifungu cha 235/1985.
Kwa upande
wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama
hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama
tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili
hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai
kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na
vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani
hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya
Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo
Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo
aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake
aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na
msaada.
Aidha
kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30
na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili
amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda
kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania
kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza
kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama
hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
0 comments: